Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu leo amefanya ziara ya kukagua mabwawa kuhifadhi ya maji na tope sumu katika Mgodi wa Barrick North Mara.
Akizungumza katika nyakati tofauti, Mheshimiwa Zungu amewashauri viongozi wa mgodi kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira na uchumi katika kutibu maji yenye sumu yanayozalishwa na mgodi huo.
“Kwa sasa tumejiridhisha usalama upo na maji taka yaliyopo pale hayawaathiri wananchi” alisema Mheshimiwa Zungu.
Aidha Mheshimiwa Zungu amewataka wachimbaji wadogo wa dhahabu kufuata utaratibu wakati wa kutumia zebaki katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.
“Utaratibu usipofuatwa, zebaki inamadhara makubwa sana kwa binadamu sio waliopo sasa hata kwa vizazi vinavyokuja” alisema Mheshimiwa Zungu.
Akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa ulipaji fidia kwa wananchi wa Nyamongo Mwenyekiti wa Kijiji cha Matongo Bwana Daudi Itembe Nyamhanga ameishukuru sana serikali kwa kumaliza kero zilizokuwa zinawakabili wananchi wa Nyamongo kwa wakati.
“Sisi wananchi wa Nyamongo wakati mwingine tunafanya ukorofi tukiona mambo yetu hayatekelezwi kama tunavyotarajia” alisema Bwana Nyamhanga.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Zungu ameambatana na Waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Esinati Chaggu pamoja na watendaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na viongozi wengine.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa