TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA ELIMU MKOA WA MARA
UTANGULIZI
Mkoa wa Mara kwa mwaka 2015 una jumla ya Shule za Awali 792 (Serikali 751, na binafsi 41), Shule za Msingi 792 (Serikali 751, binafsi 41) , Shule za Sekondari 195 (serikali 163 na 32 za binafsi), Vyuo vya Ualimu 4 ( serikali 2 na 2 vya binafsi). Pia zipo asasi za Elimu – Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Chuo cha Ufundi (VETA) na Chuo Kikuu Huria.
Mkoa una jumla ya wanafunzi wa Elimu ya Awali 75,087 (wav 37,771 was 37,316), Elimu ya Msingi 445,347 (wav 223,031 na was 222,316) Elimu ya Sekondari 77,169 (Wav 45,330 na Was 31,839)
Uandikishaji darasa la kwanza
Mwaka 2015 jumla ya wanafunzi 72,661 walitarajiwa kuandikishwa kuanza darasa la kwanza. Hadi kufikia Machi 2015 jumla ya wanafunzi 63854 (wav 32127 na was 31727) waliandikishwa kuanza darasa la kwanza sawa na asilimia 110 ya malengo.
Katika uandikishaji Mkoa bado haujafikia hatua ya rika lengwa, kwani bado kuna kundi kubwa la Watoto wanaobaki. Mkoa umefikia asilimia 92 ya rika lengwa. Hivyo Mkoa unaendelea kuzihimiza Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji kata/ mitaa kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa.
Pamoja na jitihada mbalimbali za makusudi zinazofanywa na Mkoa kwa kushirikiana na Serikali Kuu katika kuboresha miundombinu katika Sekta ya Elimu lakini bado Mkoa unakabiliwa na upungufu makubwa ya miundombinu
TAALUMA KATIKA SHULE
Shule za Msingi
Takwimu za Uendeshaji na Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi [PSLE] kwa mwaka 2013 na 2014
Shule za Sekondari
Katika kipindi cha miaka 2006 – 2015 msukumo mkubwa umeelekezwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya Shule za Sekondari za Kutwa ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kuendelea na Elimu ya Sekondari. Katika kipindi hiki jumla ya shule mpya za sekondari 25 za Kutwa zilifunguliwa. Idadi hii imetuwezesha kuwa na shule 163 za Sekondari za Serikali.Aidha, Mkoa una shule 32 zisizo za Serikali na hivyo kuufanya Mkoa kuwa na jumla ya Shule 195 za sekondari.
Jitihada za kupanua Elimu ya Sekondari
(a)Mwaka 2010 Mkoa ulifungua Shule 6 za Sekondari za Kutwa: Musoma vijijini ( Rusoli Sekondari), Tarime (Nyamisangura Sekondari, Sirari Sekondari,Korotambe Sekondari, Kemambo Sekondari na Inchage Sekondari).
(b)Mwaka 2010 Mkoa ulipata kibali cha kufungua shule ya Kidato cha Tano na Sita Wilaya ya Rorya (Nyanduga Sekondari). Pia Mkoa ulianzisha shule za Sekondari za Kidato cha Tano hadi cha Sita (A-Level) kwa kupanua Shule za Sekondari za Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (O-Level) mwaka 2011. Shule hizo kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:- Bunda (Bunda sekondari), Musoma Manispaa (Morembe sekondari), Serengeti (Machochwe sekondari na Natta sekondari), Tarime (Mogabiri sekondari), Musoma (V) (Kasoma Sekondari).
(c)Mahitaji ya Shule za Sekondari za A-Level katika Mkoa ni Shule 20 ikilinganishwa na Shule 10 za Serikali na 07 zisizo za Serikali zilizopo. Hivyo kuna upungufu wa shule 10 za A-level za Seikali sawa na 50%.
Changamoto katika shule za sekondari
•Uhaba wa walimu shuleni hususan walimu wa Hisabati, Kiingereza na Sayansi.
•Upungufu wa majengo ya shule hususan Nyumba za Walimu, Vyumba vya Madarasa, Vyoo, Maabara, Hosteli, Maktaba na Majengo ya Utawala.
•Upungufu wa samani: Madawati, Meza, Viti na Makabati.
•Uhaba wa Vifaa vya kufundishia na kujifunzia: Vitabu, Vifaa na Madawa ya Maabara.
Mahudhurio ya wanafunzi
Mahudhurio ya Wanafunzi shuleni ni wastani wa asilimia 78. Aidha utoro sugu na mimba shuleni ni 0.72% ikilinganishwa na wanafunzi wanaohudhuria masomo shuleni kwa mwaka. Juhudi zinafanyika kupambana na changamoto hizo.
Elimu ya Watu Wazima (EWW)
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoa wa Mara katika kipindi hiki imekuwa na shughuli ya kufuatilia na kufungua vituo vipya vya masomo ya jioni ya sekondari katika programu ya Elimu Masafa na ana kwa ana (ODL).
Lengo la programu hii ni kumkomboa mwananchi ambaye hakupata fursa ya kusoma shule au aliyepata matatizo na kushindwa kumaliza elimu yake katika mfumo rasmi. Utoaji wa Elimu hii katika Halmashauri zetu bado ni mdogo hivyo bado mkazo unaendelea kuwekwa.
Mikakati
•Kusajili wanafunzi wa ODL zaidi ya 1600 katika Mkoa wa Mara kwa lengo la kuwa na wastani wa wanafunzi wasiopungua 270 kwa kila Halmashauri.
•Kuhimiza ukusanyaji wa karo kabla ya usajili kwa wanafunzi wa ODL, Udereva na Kompyuta.
•Kuanzisha au kufufua vituo vya MEMKWA.
•Kuhimiza mahudhurio na kulipa honoraria kwa muda unaotakiwa.
Changamoto kwenye EWW
● Kuibuka kwa watu binafsi au vikundi visivyo na mamlaka ambavyo huendesha Elimu ya Sekondari katika mfumo usio rasmi.
● Kukosekana kwa maktaba vijijini ambazo zingeweza kutumiwa na vijana na watu wazima wanaosoma elimu ya watu wazima.
● Ukosefu wa fedha za kuendesha shughuli za EWW na vitendea kazi hivyo kupunguza ufanisi katika utoaji wa Elimu nje ya mfumo rasmi.
● Bado Halmashauri hazijaweza kukusanya takwimu sahihi za EWW.
Elimu ya Ufundi
Mkoa unatambua kuwa Elimu ya Ufundi itawasaidia sana vijana mbalimbali wanaomaliza Elimu ya Msingi na Sekondari waliokosa kuendelea na Elimu ya Juu.
Kwa kutambua hilo, Mkoa unacho Chuo cha VETA katika Wilaya ya Musoma na juhudi zinaendelea kufanyika kuhakikisha kuwa kila wilaya inakuwa na Chuo cha Ufundi kwa siku zijazo.
TAKWIMU ZA UDAHILI WA WANAFUNZI MWAKA 2012-2015
VYUO VIKUU
Chuo Kikuu Huria
•Mkoa wa Mara una Tawi la Chuo Kikuu Huria [OUT]
•Chuo kimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutoa Elimu ya Juu kwa watu mbalimbali ambao ingewawia vigumu kujiunga na Elimu ya Juu katika mfumo rasmi.
•Chuo hicho kimewawezesha wahitimu kupata ajira mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao.
Chuo Kikuu cha Arusha
Chuo hiki kimefungua Tawi lake katika Mkoa wa Mara mwaka 2009 na kimeomba kutumia majengo ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare. Chuo kimeshaanza na kina Wahadhiri na Wanafunzi.
Takwimu za Udahili wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Arusha
Mkakati wa kuboresha Elimu Mkoani
Katika mwaka huu 2015/2016, Mkoa umedhamiria kupandisha kiwango cha ufaulu kufikia 80+% sambamba na jitihada za kuongeza na kuboresha miundombinu kwa:-
•Kufanya tathmini na kujadiliana na Wadau wa Elimu kuhusu mbinu mbalimbali za kuinua kiwango cha elimu na upanuzi wa Elimu ya Sekondari hususani kwa Kidato cha Tano na Sita.
•Kuimarisha Vituo vya Walimu (TRCs) kwa kuvipatia vifaa kwa ajili ya kutoa semina kwa walimu wa masomo hususani katika mada tata.
•Halmashauri kuendelea kuziwezesha Idara za Ukaguzi kufanya kazi ya Ukaguzi ipasavyo na kufuatilia taarifa zinazotolewa kwa ajili ya kurekebisha kasoro zinazojitokeza kwa lengo la kuimarisha ufundishaji.
•Kutumia Vyuo vya Ualimu vilivyopo Mkoani mwetu (Bunda T.C, Tarime T.C. na St. Alberto T.C.) kwa ajili ya walimu wetu kupata ujuzi wa kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia na kupata mbinu za kisasa za ufundishaji.
•Kuziwezesha Kamati za Taaluma kuanzia ngazi ya Shule, Kata, Wilaya hadi Mkoa kusimamia na kuendesha shughuli zinazohusiana na uboreshaji wa Kiwango cha Taaluma; kwa mfano; Mitihani ya Majaribio, (Mock) Semina za Masomo, Mashindano ya Kitaaluma, n.k.
•Kuunda Vikosi Kazi (Task Force) za kufuatilia maendeleo ya shule kuhusu ufundishaji, mahudhurio ya wanafunzi na walimu na kuzuia vikwazo vya jitihada za Mkoa katika kuboresha Elimu kwa kutumia Sheria na Kanuni za Elimu.
•Halmashauri zetu kusisitiza uwajibikaji kwa Walimu, Waratibu Elimu Kata na pia Wazazi/Walezi katika kusimamia ufundishaji na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi shuleni na Shule zetu kwa ujumla.
MICHEZO NA UTAMADUNI
RAS Mara Sports Club
Hii ni Club ya michezo kwa watumishi walioko katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. Club hii inaunganisha Ofisi za Wakuu wa Wilaya ndani ya Mkoa. RAS-Mara Sports Club imejiunga na shirikisho la michezo ya Wizara na Idara za Serikali linalounda (SHIMIWI).
MATUKIO YALIYOPITA
Mashindano ya Darts Taifa Cup
Timu ya Darts Mkoa wa Mara ilishiriki mashindano ya Darts Taifa Cup yaliyofanyika Mkoani Mara tarehe 25-26/07/2015. Katika Mashindano hayo jumla ya Mikoa nane ya Tanzania ilishiriki na timu ya Mkoa wa Mara ilifika hatua ya fainali na kufanikiwa kushika nafasi ya pili. Timu hiyo ilipata zawadi ya kombe na fedha taslimu shilingi 25,000 wakati bingwa wa mashindano hayo alizawadiwa shilingi 50,000/= pamoja na kombe.
Mashindano ya Taifa ya riadha
Timu ya Mkoa wa Mara ilishiriki katika mashindano ya Riadha ya Taifa yaliyofanyika tarehe 05-07/06/2015 Jijini Dara Es Salaam. Timu hiyo ilikuwa na jumla ya wanariadha wanne ambao walifanikiwa kupata medali mbili za shaba na fedha.
Mashindano ya Netiboli Mkoa
Chama cha Mpira wa Netiboli Mkoa wa Mara (CHANEMA) kiliandaa Mashindano ya Mkoa kwa lengo la kuchagua timu ya Mkoa itakayoshiriki mashindano ya ligi ya netiboli daraja la pili ngazi ya Taifa mwezi Oktoba Mkoani Kagera. Mashindano hayo yalifanyika tarehe 01/08/2015 Manispaa ya Musoma. Jumla ya wachezaji 24 walichaguliwa kuunda timu ya Mkoa.
Mashindano ya Mkoa Ligi Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa
Mashindano ya klabu bingwa ya Mkoa yalifanyika mwezi Machi 2015. Timu ya Baruti Football Club iliibuka mabingwa wa Mkoa katika mashindano hayo. Timu hiyo iliuwakilisha Mkoa katika mashindano ya Mabingwa wa Mikoa yaliyofanyika Mkoani Manyara na kushika nafasi ya nne.
Mafunzo ya walimu wa Michezo Mkoa wa Mara
Walimu wa michezo Mkoa wa Mara kwa shule za Msingi na Sekondari walishiriki kwenye mafunzo ya michezo yaliyohusisha mchezo wa mpira wa miguu, netiboli, voleboli na mpira wa mikono. Jumla ya walimu 55 walishiriki mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 02-07/03/2015 katika Chuo cha Ualimu Bunda.
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)
Mashindano ya 37 ya UMISSETA ngazi ya Mkoa yalifanyika katika Chuo cha Ualimu Tarime kuanzia tarehe 23-25/05/2015.
Katika Mashindano ya Kanda Mkoa wa Mara ulipata ushindi wa kwanza katika mchezo wa Mpira wa miguu wavulana, Mpira wa miguu wasichana, Mpira wa Mikono wavulana pamoja na Kwaya. Timu hiyo ya Kanda ilipata vikombe 05 katika michezo mbalimbali ambayo ni Soka wavulana na wasichana, riadha wavulana, mpira wa mikono wasichana na wavulana.
Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA)
Mashindano ya 21 ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yalifanyika katika Chuo cha Ualimu Tarime kuanzia tarehe 12-14/06/2015. Timu ya Mkoa wa Mara ilipata jumla ya medali 11 ambazo ni dhahabu 01, shaba 02 na fedha 08 na kikombe cha mshindi wa pili mchezo wa netiboli. Mashindano ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2015 ngazi ya Taifa yaliratibiwa kimkoa na sio kikanda.
Mtihani wa Mock Kidato cha Nne
Mtihani wa Mock Kidato cha Nne Mkoa wa Mara ulifanyika kuanzia tarehe 20/07-03/08/2015. Baada ya kumalizika kwa mtihani huo zoezi la usahihishaji lilifanyika na kukamilika kama ilivyokusudiwa.
SEMINA YA EQUIP ‘’STRATEGIC PLAN I
Semina iliandaliwa na EQUIP kwa Maafisa Elimu wa Wilaya na Maafisa Mipango juu ya uaandaaji wa Mpango Mkakati wa kuinua ubora wa Elimu. Semina hii ilifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
SEMINA YA EQUIP STRATEGIC PLAN II
Semina iliandaliwa na EQUIP kwa Maafisa Elimu wa Wilaya na Maafisa Mipango juu ya uaandaaji wa Mpango Mkakati wa kuinua ubora wa Elimu. Semina hii ilifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Katika Mkoa wa Mara EQUIP inafanya shughuli zifuatazo ni:-
i)Kuinua kiwango cha utendaji wa walimu
ii)Kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule
iii)Kuimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi za Mikoa na Wilaya
iv)Kuimarisha ushiriki wa jamii katika maendeleo ya elimu
v)Ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa taarifa za kielimu.
SEMINA YA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA UTAMBULISHO WA MUHTASARI WA DARASA LA I NA II
Semina ya Mtaala wa Elimu ya Awali na Utambulisho wa Muhtasari wa darasa la I na II iliendeshwa na EQUIP-T na kuwashirikisha Maafisa Elimu wa Wilaya pamoja na Wakaguzi wa Shule Mkoa wa Mara. Semina hii ilifanyika mwezi Julai 2015 katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara akifungua Semina ya Mtaala wa Elimu ya Awali na utambulisho wa Mihtasari ya darasa la I na II katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.
SEMINA YA UTAYARI WA KUANZA SHULE
Semina hiyo iliandaliwa na EQUIP-T na kuwashirikisha Maafisa Elimu wa Wilaya. Lengo la semina hiyo lilikuwa ni kutoa stadi zitakazo wawezesha wasimamizi wa Elimu katika Wilaya kuandaa mafunzo yatakayo wawezesha wanafunzi walio nje ya Mfumo wa Elimu ya Awali kupata mafunzo ya wiki 12 ili waweze kuandikishwa darasa la kwanza.
MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI (PSLE) 2015
Maandalizi ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) yako katika hatua za mwisho. Mtihani unatarajiwa kufanyika tarehe 09 na 10/09/2015 .
Jumla ya watahiniwa 43,359 kutoka Halmashauri zote nane za Mkoa wa Mara wakiwemo wavulan 21,630 na wasichana 21,729 wanatarajiwa kufanya mtihani huo kutoka shule 761 zikiwemo 730 za mfumo wa Kiswahili zenye watahiniwa 42,512 (wav. 21,165 na was. 21,347) na 31 za mfumo wa Kingereza zenye watahiniwa 847 ( wav. 465 na was.382). Watahiniwa watafanya mtihani wa Somo la Sayansi, Hisabati Kiswahili, Kingereza na Maarifa ya Jamii kwa Shule za mfumo wa Kiswahili na Science, Mathematics, Kiswahili, English na Social Studies kwa shule za mfumo wa Kingereza. Mchanganuo wa watahiniwa kwa kila Halmashauri .
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa