Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kifupi TEHAMA ni moja kati ya vitengo vitano (5) vikiwemo vya Sheria, Ukaguzi wa Ndani, Uhasibu na Ununuzi na Ugavi vilivivyoanzishwa baada ya Serikali kufanya marekebisho ya Muundo wa Sekretarieti za Mkoa ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Mrisho Jakaya Kikwete alisaini waraka wa Serikali uitwao The Functions and Organisation Structure of the Regional Secretariats tarehe 3 Juni, 2011.
Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Kitengo cha TEHAMA ilikuwa ni kutoa utaalam na huduma katika maeneo yote yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Sekretarieti ya Mkoa. Ikumbukwe tu kuwa TEHAMA ni moja kati ya sekta inayojitegemea, lakini pia ni sekta mtambuka ambapo inaziwezesha sekta nyingine za kiuchumi na kijamii kazi zake za ufanisi. Ili kuelewa zaidi kuhusu majukumu ya Kitengo cha TEHAMA, bonyeza hapa.
MIUNDOMBINU YA TEHAMA
Kitengo cha TEHAMA kimesimika na kinasimamia Mtandao wa Ndani wa Mawasiliano – Local Area Network (LAN) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo mtandao huu unatumika kuzifikishia Sehemu na Vitengo huduma ya Internet.
MIFUMO YA KOMPYUTA
Kitengo cha TEHAMA katika Sekretarieti ya Mkoa ni msimamizi na mshauri mkuu katika ngazi ya Mkoa kuhusu masuala ya TEHAMA katika Sekretarieti yenyewe na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizoko mkoani Mara. Kitengo cha TEHAMA kinasimamia mifumo ya Intergrated Financial Management Information System – IFMIS/Epicor, Human Capital Management Information System – HCMIS/Lawson, Intergrated Tax Management – iTAX, Planning and Reporting System – PLANREP, LGMD na mifumo mingine mingi ambayo imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kazi fulani.
TOVUTI YA MKOA
Sekretatieti ya Mkoa wa Mara ina tovuti ambayo hutumika kutoa taarifa na elimu kwa yeyeto yule atayaeifungua. Tovuti hii iitwayo www.mara.go.tz ina kurasa zenye taarifa na matukio yanayotokea katika Mkoa wa Mara, lakini zipo kurasa maalum za Mamlaka za Serikali za Mitaa zinazoelezea Mamlaka hizo.
Tovuti ya Mkoa inatoa huduma ya barua pepe kwa Sehemu, Vitengo na maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanazozitaka taasisi za Serikali na Wakala wake kutumia barua pepe zinazotokana na tovuti za taasisi hizo ili kuimarisha upatikanaji bora wa mawasiliano na usalama wa taarifa zenyewe.
Hivi karibuni, tovuti ya Mkoa wa Mara itaboreshwa na kuongeza taarifa nyingi zinazohusu Sekretarieti ya Mkoa yenyewe na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuifanya Serikali kuwa wazi zaidi kwa kutoa taarifa (Open Data). Taarifa zitakazowekwa ni pamoja na Mipango na bajeti, taarifa za utekelezaji, mapokezi ya fedha, matokeo ya zabuni, taarifa za uhamisho n.k.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa