• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

Posted on: January 6th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 06 Januari, 2026 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) ambacho pamoja na mambo mengine kimepokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto awamu ya pili na kuagiza Wilaya na Halmashauri kuhakikisha ukeketaji inakuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyote.

Mhe. Mtambi ametoa agizo hilo kufuatia taarifa kuwa nguvu ya mila na desturi kandamizi ikiwemo ukeketaji na mfumo dume bado ni kikwazo katika utekelezaji wa mpangokazi huo hata baada ya Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kutoa elimu kwa muda mrefu lakini bado ukeketaji unafanyika katika jamii na hususan Wilaya za Tarime na Serengeti na wilaya nyingine kwa wananchi wenye asili ya kabila la Wakurya.

“Ninaagiza ukeketaji ujadiliwe kwenye vikao vyote ngazi ya Wilaya na Halmashauri ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili ambalo linarudisha nyuma juhudi za serikali katika kutoa kufikia usawa wa kijinsia katika nchi yetu” amesema Mhe. Mtambi.  

Kanali Mtambi ameiagiza Sekretarieti ya Mkoa kuhakikisha Wilaya na Halmashauri zote zinaendesha midahalo, makongamani na mijadala katika jamii kuhusiana na namna ya kukomesha suala hili katika Mkoa wa Mara na kutoa hadi tarehe 30 Januari, 2026 majadiliano hayo yawe yameanza.

Kanali Mtambi amewataka viongozi na watendaji kuwahusisha wazee wa kimila, machifu, mangariba na viongozi wa dini katika kupambana na suala la ukeketaji ili kuleta mabadiliko yanayotarajiwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania Ndugu Rhobi Samweli amesema tatizo la ukeketaji linaendelea katika jamii kwa sababu ngozi inayotolewa wakati wa ukeketaji inatumika katika jamii kwa Imani kwa inakuza biashara.

“Ngozi inayotolewa katika ukeketaji ni biashara kubwa katika jamii na inatumika kwa imani kuwa inakuza na kulinda biashara” amesema Mhe. Rhobi na kuongeza kuwa biashara kubwa zinazotumia ngozi hiyo kuwa ni uchimbaji wa madini, kilimo, uvuvi na maduka.

Ndugu Rhobi amesema kutokana na biashara hiyo inakuwa vigumu kutokomeza suala la ukeketaji wakati kuna watu wanaonufaika na biashara ya ngozi inayotolewa wakati wa ukeketaji na kuitaka Serikali kusimamia kwa karibu kukomesha vitendo vya ukeketaji.

Kwa upande wake, Mbunge wa Tarime Vijijini Mhe. Mwita Waitara amesema suala la ukeketaji ni suala lililozoeleka la kimila na kiutamaduni na limekuwa linafanyika kwa muda mrefu na inakadiliwa kuanzia miaka ya 1800 na kuitaka Serikali na wadau wa maendelo kuendelea kutoa elimu ili kupata mabadiliko ya kweli ya jamii.

“Hatutegemei suala hili watu waliache siku moja, wanaliacha taratibu na tayari baadhi ya watu wameacha lakini wengi wao wanaendelea kukeketa wasichana na wavulana” amesema Mhe. Waitara.

Aidha, ameitaka Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kuwekeza zaidi katika kutoa elimu kwa wanaume kwani kwa sasa elimu wanapewa zaidi wanawake ambao kwa maoni yake hawana sauti nyumbani kwao na katika jamii zao.

Mhe. Waitara amesema kwa sasa hata baadhi ya desturi zimebadilika hapo awali mwanamke asiyekeketwa alikuwa anatengwa katika shughuli zote za kijamii lakini utoaji wa elimu na kuenea kwa shule za kata kumesaidia wananchi kuweza kubadilisha mtizamo kwa haraka.

Aidha, amezitaka nyumba salama kuwatumia kama mifano watu wengine kutoka katika jamii ambao hawajakeketwa na watoto wanaokimbia ukeketaji kuwatunza hadi wakiwa wakubwa ili wakirudi wamejitegemea wawe mfano kwa wananchi wengine kuona kuna maisha mazuri nje ya ukeketaji na kuonya kuwa wakiwarudisha ndani ya muda mfupi wanaenda kukeketwa tena.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto awamu ya pili, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Jamii Mkoa wa Mara Ndugu Neema Ibamba amesema utekelezaji wa mpango huo katika Mkoa wa Mara umejikita katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji.

Bibi Ibamba amesema maeneo hayo ni uanzishwaji wa sheria ndogo ndogo za kuzuia ukatili, uinuaji wa wanawake kiuchumi, ufanyaji wa vikao vya ujirani mwema kati ya Tanzania na Kenya, uimarishaji wa utendaji kazi wa Kamati za MTAKUWWA, mijadala na midahalo ya makundi rika katika jamii, uimarishaji wa mfumo wa udhibiti wa ukatili.

Maeneo mengine ni uanzishwaji wa madawati ya ulinzi na usalam shuleni, kutambua na kutoa mafunzo kwa watu wa kuaminika, viongozi wa dini na kutoa mikopo na kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa afua za WWU.

Ndugu Ibamba amesema kuanzishwa kwa kamati za MTAKUWWA katika ngazi mbalimbali hadi Kata na Vijiji imeimarisha ufuatiliaji na uratibu wa afua za kupinga ukatili katika jamii.  

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, wabunge, Meya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara, Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa, maafisa kutoka taasisi za umma, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kiraia.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Mara yaazimia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa