KUHUSU IDARA/SEKSHENI
Seksheni hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
MAJUKUMU YA IDARA/SEKSHENI
Majukumu ya Seksheni ya Miundombinu ni pamoja na:
SHUGHULI NDANI YA MIUNDOMBINU ZINAZOTEKELEZWA
UJENZI NA UKARABATI WA BARABARA
Mkoa wa Mara una mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 5,036.74 zinazohudumiwa na Mamlaka mbalimbali
BARABARA KUU/MKOA
Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara inahudumia Barabara Kuu na za Mkoa zenye jumla ya urefu wa kilomita 1,273.48. Kati ya hizo kilomita 411.61 ni Barabara Kuu na kilomita 861.87 ni Barabara za Mkoa. Kwa upande wa Barabara kuu kilomita 170.06 ni za lami na kilomita 241.55 ni za changarawe; wakati kwa upande wa Barabara za Mkoa kilomita 34.97 ni za lami na kilomita 826.90 ni za changarawe/udongo. Wakala unahudumia jumla ya madaraja 292, ambayo yapo kwenye Barabara Kuu na za Mkoa.Kwa undani zaidi kuhusu barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS), bonyeza hapa, bonyeza hapa.
MIRADI MBALIMBALI YA UJENZI WA BARABARA INAYOTEKELEZWA KATIKA MKOA WA MARA
1: UKARABATI WA BARABARA YA SIMIYU /MARA MPAKANI–MUSOMA (KM 85.5)
Ukarabati kiwango cha lami barabara ya mpakani mwa Simiyu/Mara hadi Musoma kwa gharama ya Shilingi 85.368 Bilioni. Ukarabati huo umekamilika kwa asilimia 99% (Km. 85) kazi zinazoendelea ni ujenzi wa mifereji na kuweka alama za barabarani. Ukarabati huo ulihusisha pia ujenzi wa madaraja makubwa ya Rubana (upana wa mita 70) na Suguti (upana wa mita 40) ambayo tayari yamekamilika.
2: UJENZI KIWANGO CHA LAMI BARABARA YA MAKUTANO JUU–NATTA-MUGUMU–LOLIONDO–MTO WA MBU (KM 452) MAKUTANO JUU – SANZATE KM 50
Serikali inajenga barabara hii kwa kiwango cha lami kutoka Mara (Makutano Juu) hadi Arusha (Mto wa Mbu) kwa awamu. Awamu ya kwanza ya ujenzi huu ni kwa upande wa mkoa wa Mara inahusisha sehemu ya kuanzia Makutano Juu hadi Sanzate kilomita 50. Kazi ilianza Oktoba 2013 na inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 24. Kazi hii inatekelezwa na ubia wa makampuni kumi ya kizalendo, ujulikanao kwa jina la Mbutu Bridge JV, na inasimamiwa na mhandisi mshauri M/s UWP Consulting (T) Ltd kwa ushirikiano na kampuni ya UWP Consulting (Pty) Ltd ya Afrika ya Kusini.
Kazi zinazoendelea kufanyika ni pamoja na ujenzi wa daraja la KYARANO (upana wa mita 36), Kunyanyua tuta la barabara na ujenzi wa makalvati.
3: UJENZI KIWANGO CHA LAMI BARABARA YA NYAMUSWA–BUNDA-KISORYA-NANSIO KM 121.9: SEHEMU YA BULAMBA–KISORYA (KM 51).
Serikali inajenga barabara hii kwa kiwango cha lami kutoka Nyamuswa hadi Nansio kwa awamu. Awamu ya kwanza ya ujenzi huu inahusisha sehemu ya kuanzia Bulamba hadi Kisorya kilomita 51. Kazi ilianza Desemba 2013 na inatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 24. Kazi hii inatekelezwa na kampuni ya kizalendo, ijulikanayo kwa jina la Nyanza Roadworks Ltd ya Mwanza na inasimamiwa na Meneja wa wakala wa barabara Mkoa wa Mara kwa muda hadi Mhandisi mshauri atakapopatikana.
Kazi zinazoendelea kufanyika ni pamoja na ujenzi wa makalvati makubwa na madogo, Kusafisha eneo la barabara, Kunyanua tuta la barabara na kusaga kokoto
4: UKARABATI/UJENZI WA KIWANGO CHA LAMI BARABARA YA MAKOKO.
Barabara hiyo yenye urefu wa km 6 kutoka Makutano ya Peninsula hadi Makoko,ni ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, na inajengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mara. Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka tangu 2009-10 ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa Barabara hii. Mpaka sasa Km 1.8 zimekamilika kwa kiwango cha lami. Mwaka wa fedha 2014/15 Serikali ilitenga jumla ya Shilingi 1.125 ilioni kwa ajili ya kipande cha kilomita 1.4.
5: UPEMBUZI YAKINIFU NA USANIFU WA KINA WA BARABARA YA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKELA 92km.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/15, Serikali kupitia mfuko wa barabara (Roads Fund) ilitenga jumla ya Shilingi 400.00 milioni kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika barabara tajwa. Taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri kwa kazi hiyo zimekamilika na mkataba umeshasainiwa.
6: MATENGENEZO MAKUBWA BARABARA YA MAKUTANO (ZIROZIRO)-SIRARI (KM 84).
Kuwekewa tabaka gumu la lami kuimarisha uhai wa barabara hii kwa miaka mingine 10 hadi 15 unaendelea kwa awamu. Katika mwaka wa fedha 2013/14 zimefanyika km 10.78 kwa gharama ya bilioni 2.99. kwa sasa km 42.8 zimekamilika kuwekewa tabaka gumu la lami. Uboreshaji wa barabara hii unahusisha pia kuimalisha nyaya zinazoshikilia daraja la Kirumi (Kirumi cable – stayed Bridge) lililojengwa kati yam waka 1984 – 1985.
7: UKARABATI WA BARABARA YA MIKA-UTEGI-SHIRATI.
Barabara hiyo inaunganisha makao makuu ya wilaya ya Rorya na barabara kuu ya Makutano (ZIROZIRO)-Sirari. Katika mwaka wa Fedha 2013/14 zilijengwa km 0.35 kwa gharama Shilingi milioni 352.69. Hadi sasa km 6.65 zimekamilika.
BARABARA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA
Mkoa wa Mara una mtandao wa barabara zenye urefu wa jumla ya kilomita 3,759.25 zinazo hudumiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya za Bunda, Serengeti, Rorya, Tarime,Tarime Mji, Butiama na Musoma na Manispaa ya Musoma). Matengenezo ya barabara hizi hutegemea vyanzo mbalimbali vya fedha, kiasi kikubwa kikitoka Mfuko wa barabara. Kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Mkoa wetu ulipanga kufanya matengenezo katika barabara hizi kwa urefu wa kilomita 1,339.64, vivuko 259 na madaraja 4 kwa gharama ya Tshs 10,924.774 toka Mfuko wa Barabara, fedha za dharura, Miradi ya Maendeleo, Mpango wa Uimalishaji Miji na Manispaa Nchini (Urban Local Government Strengthening Program) na fedha za mapato ya ndani (Own Source). Pata mchanganuo wa mategengenezo ya barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi cha miaka mitano (2010-2015) kwa kubonyeza Bunda, Butiama, Musoma, Manispaa ya Musoma, Rorya, Serengeti, Tarime au Tarime Mji
VIVUKO VILIVYOPO MKOA WA MARA
Mkoa wa Mara kwa sasa una vivuko viwili ambavyo ni MV-Musoma na MV-Mara. Kivuko cha MV-Musoma kinatoa huduma kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Kijiji cha Kinesi katika Halmashauri ya Wilaya Rorya. Kivuko cha MV-Mara kinatoa huduma kati ya Mugara (Wilaya Bunda) na Kurugee (Wilaya Butiama
HALI YA VIVUKO
Vivuko vyote viwili viko katika hali nzuri na vinaendelea kutoa huduma kama kawaida. Kivuko cha MV-Musoma kinafanya safari zake mara nne kwa siku na MV-Mara kinafanya safari mara tatu kwa siku.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa