Wilaya ya Rory ni miongoni mwa Wilaya 6 za Mkoa wa Mara. Wilaya ya Rorya ilianza rasmi tarhe 01/07/2007 baada ya kugawanywa kutoka Wilaya ya Tarime ikiwa na Tarafa 4, Kata 21, vijiji 81 na Jimbo 1 (Rorya) la Uchaguzi
Mkuu wa Wilaya wa kwanza ni Mhe. Lt. Kanali (MST) Benedict K. Kitenga na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya alikuwa Bw. Jacob A. Kayange kati ya 1.07.2007 na 19.11.2009.
Wilaya ipo Kaskazini mwa Tanzania kati ya Latitude 1⁰.00˝ hadi 1⁰ 4.5˝ Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudi 33⁰.30˝ hadi 35⁰.00˝Mashariki mwa mstari wa Meridian. Wilaya ina ukubwa wa kilometa za mraba 9,345.496 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo:-
Eneo la maji [Ziwa Victoria] kilomita za mraba 7,252 sawa na 77.6%, eneo la ardhi [Nchi kavu] kilomita za mraba 2,093.496 sawa na 22.4%. Wilaya inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Tarime kwa upande wa Mashariki, Wilaya ya Musoma Vijijini kwa upande wa Kusini na Nchi ya Uganda kwa upande wa Magharibi.
Mgawanyo wa Wilaya Kiutawala: Kiutawala, Wilaya ya Rorya kwa sasa inaundwa na Tarafa nne (4), Kata ishirini na sita (26) na Vijiji themanini na saba (87) na Vitongoji 509.
Jedwali1: Historia ya Viongozi wa Wilaya ya Rorya
Na.
|
Jina Kamili
|
Mwaka alioanza
|
Mwaka aliondoka
|
1.
|
Simon K.Chacha
|
2016
|
-
|
2.
|
|
|
|
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa