Vituo vya Kutolea Huduma za Afya: Mkoani Mara Zahanati zimeongezeka kutoka 221 mwaka 2010 hadi 241 mwaka 2015 kati ya hizo 26 ni za mashirika ya dini na 27 ni za watu binafsi sawa na ongezeko la asilimia 9. Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 36 mwaka 2010 hadi 41 mwaka 2015 ambapo 6 ni vya mashirika ya dini na 7 sekta binafsi sawa na ongezeko la asilimia 13. Mkoa wa Mara unatekeleza mpango wa maendeleo wa afya ya msingi (MMAM) tangu mwaka 2007. Hadi kufikia mwaka 2015 Mkoa umetumia Tsh. 4,369,742,665/= na umeweza kujenga Zahanati 50, Vituo vya Afya 3,Nyumba za watumishi 33 na kukarabati Zahanati 91, Vituo vya Afya 18 na nyumba za watumishi 37. Bado mkoa haujafikia lengo ambapo hadi kufikia 2015, Mkoa una jumla ya vijiji na mitaa 673, vyenye zahanati ni 241 ambayo ni asilimia 36 na Kata 171 zenye vituo vya afya ni 41 (ambayo ni asilimia 24), hii inachangiwa na ufinyu wa rasilimali fedha.
Aidha ili kuhakikisha kuwa Mkoa unakuwa na Hospitali ya rufaa yeye miundombinu, vifaa tiba na wataalam wa kutosha kutoa huduma za Kibingwa katika fani zote muhimu, Uongozi wa Mkoa umeamua kuendeleza ujenzi wa jengo la hospitali ya Kwangwa ili iwe Hospitali ya rufaa ya Mkoa itakayoitwa Mwalimu Nyerere Medical Centre. Kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2013/2014 – Serikali ilitenga kiasi cha shilingi 4.2 bilioni na pia kutenga kiasi cha shilingi 2.1 bilioni mwaka 2014/2015. Hadi sasa mkoa umepokea jumla ya Tsh 3,334,967,000 katika bajeti ya serikali kwa ajili ya mradi huu kwa mwaka 2012/2013 na 2013/2014 .Kazi zilizofanyika 2014/2015 ni pamoja na:-
Mwonekano wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere
Watumishi wa afya wa Serikali katika Mkoa wameongezeka toka 1,307 mwaka 2010 hadi 2424 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 85.5 Kwa mfano Madaktari bingwa mwaka 2010 walikuwa 3 na mwaka 2015 wako 8, Wauguzi wenye shahada (BSc Nursing) mwaka 2010 hawakuwepo na mwaka 2015 wako 18 na Madaktari (MD) mwaka 2010 walikuwa 10 na mwaka 2015 wako 23.
Bado kuna changamoto ya upungufu wa watumishi, kwani waliopo ni asilimia 65 tu ya mahitaji. Sababu za upungufuu huu ni watumishi kutopenda kuja Mkoa wa Mara na wanaokuja huhama baada ya muda mfupi. Katika kukabiliana na tatizo hili Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri unatumia mbinu na mikakati mbalimbali ili kuvutia watumishi kuja Mara na kuwabakiza. Mikakati hiyo ni pamoja na motisha kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuwapa stahili zao kwa wakati.
Mkakati wa Mkoa wa kuboresha Afya ya mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto
Mkoa una Mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga unaoendelea kutekelezwa. Lengo kuu la mkakati huu ni kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka 91 mwaka 2013 hadi 40 mwaka 2016. Malengo mahususi ni pamoja na:
Hadi sasa Mkoa umenunua pikipiki kwa Maafisa Tarafa kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mkakati huu na kupata takwimu sahihi katika ngazi za vitongoji,vijiji na kata na ujenzi wa Kituo cha Damu salama cha Mkoa katika hospitali ya Mkoa umeanza .
Mafanikio yameonekana katika ongezeko la matumizi ya uzazi wa mpango, yameongezeka toka 18% mwaka 2010 hadi 40% mwaka 2015, kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya imeongezeka toka 37% mwaka 2010 hadi 63% mwaka 2015.
Maboresho ya vituo 13 (Musoma Manispaa – Nyasho; Musoma DC– Murangi; Butiama DC – Kiagata; Bunda DC– Kasahunga, Ikizu na Manyamanyama; Tarime DC – Nyamongo, Muriba na Nyarwana; Rorya DC – Kinesi na Utegi; Serengeti DC – Natta na Iramba) yamekamilika kwa asilimia 95.
Vifo vya wazazi vimepungua kutoka 110/100,000 (2010) mpaka 101/100,000 (2015), kiwango cha vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi viko chini ukilinganisha na viwango vya kitaifa ambavyo mwaka 2010 kitaifa ilikuwa ni 578/100,000 hadi kufikia 454/100,000 mwaka 2015 kitaifa.
Mkoa umepata wadau MCSP – Jhpiego, Engenderhealth, Marie Stopes wa kushirikiana nao katika kutekeleza mkakati huu.
Huduma ya Watoto chini ya Miaka Mitano
VVU/UKIMWI
Mkoa wa Mara umefanya juhudi kubwa katika kupanbana na tatizo la VVU/UKIMWI.
Lengo kuu la Mkoa ni kutokomeza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI ifikapo mwaka 2016: Ili kufikia lengo hili Mkoa unatekeleza mambo yafuatayo:
Mikakati hii imeweza kupunguza maambukizi ya VVU kutoka asilimia 7.7 mwaka 2007 hadi 4.5 mwaka 2012.
Upatikanaji wa Dawa na vifaa Tiba Katika kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi muhimu kwa kipindi cha 2014/2015 Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri, wadau wa afya (CSSC, AIDS Relief) na MSD umeunda kikosi kazi (Technical working group) ambacho kimeimarisha mawasiliano kuhusu upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kuhakikisha vinakuwepo kwenye vituo vya kutolea huduma muda wote. Mawasiliano hayo yameimarishwa kwa kutumia mfumo wa watsup group. Nia ni kufahamu uhaba na upatikanaji wa bidhaa ili kuweza kugawa upya bidhaa zilizopo kulingana na uhitaji. Upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi katika vituo vya kutolea huduma umeboreka kutoka asilimia 66 mwaka 2010 hadi asilimia 75 mwaka 2015.
Kuboresha Huduma za Hospitali za Mkoa na Halmashauri
Katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali ya Mkoa mambo yafuatayo yamefanyika kwa mwaka 2014/2015;
Katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali za Halmashauri mambo yafuatayo yamefanyika kwa mwaka 2014/2015;
Mfuko wa Afya ya Jamii
Mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii. Juhudi zinazofanywa kuhakikisha kuwa kazi hii inakuwa na mafanikio ni pamoja na kuhakikisha kuwa Vituo vya kutolea huduma vinakuwa na madawa ya kutosha pamoja na kuongeza uhamasishaji kwa kushirikiana na NHIF. Hadi sasa Kaya zilizojiunga na mfuko wa Afya ya Jamii kati ya asilimia 2 (Tarime TC) na 44.2 (Musoma DC) – Kimkoa ni asilimia 10. Mchanganuo wake unaonekana katika jedwali lifuatalo:
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa