Afisa anayeshughulikia kilimo cha zao la pamba Mkoa wa Mara Eng. Okayo Mwita amewahimiza Maafisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kuhakikisha wakulima wanasaidiwa ili kuweza kufikika lengo la mavuno tulilojiwekea kama Mkoa. Eng.Okayo aliyasema hayo leo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa kulima zao la pamba katika Wilaya ya Rorya ikiwa ni agizo la Mhe.Kassimu Majaliwa(Mb) Waziri Mkuu wa Tanzania kuwa Mikoa yote inayolima pamba kuhakikisha wakulima wanawezeshwa na kusaidiwa na wataalam wa kilimo.
''Ni lazima kuhakikisha wakulima wanapewa pembejeo zitakazotosheleza mahitaji yao ili tuweze kupata mavuno mengi na yenye tija kwa mkulima na Taifa kwa ujumla" alisema Eng. Okayo.
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya ndugu Dominic Ndyetabura alisema kuwa wakulima wengi wameitikia wito wa Serikali wa Kulima zao la pamba na jumla ya hekari 366 ya zao la pamba zimelimwa katika Wilaya ya Rorya msimu huu wa Kilimo. "Ni jukumu letu kama maafisa Kilimo kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo zote zinazohitajika japokuwa kuna changamoto za hapa na pale" alisema ndugu Dominic.
Katika msimu huu wa kilimo Wilaya ya Rorya inatarajiwa kuvuna tani 366 .Hili ni ongezeko kubwa sana ukilinganisha na msimu uliopita.Kilimo cha zao la pamba ni mkombozi mpya kwa wakulima wa Mkoa wa Mara. Hili ni kutokana na mahitaji makubwa ya pamba na tayari wawekezaji wengi wameonesha nia ya kununua pamba msimu wa mavuno ujao. Kupitia zao hili wakulima wanaweza kujikwamua kutoka kwenye umasikini endapo watalima kwa bidii na kuendana na sera ya Tanzania ya Viwanda kwa kuwa tayari Serikali iko tayari kuhakikisha kilimo hiki kinaleta faida kwa mkulima.
Zao la pamba ni muhimu kwa Tanzania ya Viwanda, tulime kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa