Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa leo tarehe 28 Mei, 2023 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Tarafa ya Ingwe, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa vijiji 7 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA).
Katika ziara hiyo Mhe. Mchengerwa amepokelewa katika Kijiji cha Gibaso na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Kanali Michael Mtenjele na viongozi na watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Mara.
Wengine walioshiriki katika mapokezi na ziara hiyo ni Mbunge wa Tarime Vijiji Mhe. Mwita Waitara na wabunge wa viti maalum Mkoa wa Mara.
Katika ziara hiyo Mhe. Mchengerwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bwana Anderson Mutatembwa na Kamishna wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Bwana William Mwakilema.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mchengerwa amepokea taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na zoezi la uwekaji wa vigingi vya mpaka kati ya vijiji vya Tarafa ya Ingwe na SENAPA na amezungumza na wananchi wa Tarafa ya Ingwe katika vijiji vya Gibaso na Kegonga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa