• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Watumishi na Bodi ya Barabara Mara wapewa elimu ya bima

Posted on: March 4th, 2025

Mamlaka ya Usimamia wa Bima Tanzania (TIRA) leo imetoa elimu ya bima kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji.  

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha mali, vifaa na magari ya serikali yanakatiwa bima ili kulinda mali za Serikali na majanga yanayoweza kutokea.

“Hili suala la bima kwa mali za Serikali ni muhimu sana, majengo, magari na mali nyingine za Serikali zinapopata ajali inakuwa ni hasara kubwa kwa Serikali na mara nyingi zinakuwa hazitumiki tena” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka wajumbe kufuatilia mafunzo hayo ya bima na baadaye kwenda kutoa elimu ya bima kwa wananchi wanaowaongoza ili waweze kujua umuhimu wa bima na namna ya kufaidika na fursa za bima.

Mhe. Mtambi amesema bima kama ya kilimo inaweza kuwasaidia wananchi wengi kuwekeza kwenye kilimo wakiwa na uhakika wa kupata mazao hata kama msimu huo kilimo kikiwa sio kizuri baada ya kukata bima ya kilimo.

“Hii bima ya kilimo ni muhimu sana kwani wananchi wengi wanapata hasara kubwa baada ya kuwekeza na kupata majanga mbalimbali jambo ambalo mkulima huyo akiwa na bima linaepukika” amesema Mhe. Mtambi.

Aidha, Mhe. Mtambi amewataka wajumbe wa kikao hicho kuwahamasisha wananchi kukata bima za afya ili kuwasaidia kupata matibabu ya uhakika wakati wanapokumbwa na magonjwa au ajali na kuhitaji matibabu.

Awali, akiongoza kikao cha mafunzo ya watumishi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara ameishukuru TIRA kwa kutoa elimu ya bima kwa watumishi na kuwataka watumishi kuchangamkia fursa hiyo na kuwekeza katika masuala ya bima.

“Hii ni fursa nzuri kwa watumishi ambayo inawawezesha kuwa wateja wa bima mbalimbali zilizopo hapa nchini pamoja na kuwa wawekezaji katika sekta hii ya bima hata kama bado unaendelea na kazi yako” amesema Bwana Kusaya.

Bwana kusaya amewataka watumishi  wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kufuatilia kwa umakini mafunzo hayo na kuuliza maswali kupata uelewa na baadae kuchukua hatua katika kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware amewataka watumishi wa Serikali na viongozi kutoa ushirikiano kuweza kufanikisha malengo ya Serikali katika kuhakikisha asilimia 50 ya wananchi wanakuwa na bima.

Dkt. Saqware amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha mali za Serikali zilizopo kwenye maeneo wanayoyasimamia zinawekewa kinga ya kibima ili kuiepushia Serikali hasara inayoweza kutokea inapotokea ajali ya aina yoyote ile.

Aidha, Dkt. Saqware amesema TIRA inatoa huduma ya ushauri katika masuala ya bima kwa mali na miradi ya Serikali na kuwahakikishia viongozi kuwa TIRA itatoa ushirikiano kama itaombwa ushauri kuhusiana na masuala ya bima.  

Dkt. Saqware amesema TIRa kwa mujibu wa sheria inayo majukumu ya kutoa leseni na kusajiri kampuni za bima, inatakiwa kufuatilia uendelevu wa bima hapa nchini, inapaswa kulinda haki za wateja wa bima pamoja na kutoa elimu ya bima kwa wananchi.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC azitaka Wilaya kuongeza nguvu maandalizi ya Mwenge 2025

    May 09, 2025
  • Mtambi akabidhi tuzo na kinyago washindi wa Mwenge 2024

    May 09, 2025
  • Mtambi alitaka jukwaa la ushirika kuongeza ubunifu

    May 08, 2025
  • Jumuiya ya Waislamu Musoma yachangia madawati

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa