Jumla ya watahiniwa 4,225 leo wameanza kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita na vyuo vya ualimu kwa mwaka 2024 katika Mkoa wa Mara.
Kati ya watahiniwa hao, 3,591 ni wanafunzi wa Kidato cha Sita na wengine 634 ni wanachuo wa vyuo vya ualimu vitatu vilivyopo katika Mkoa wa Mara.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Makwasa Bulenga imeeleza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya kitaifa, mtihani huo unaanza tarehe 06 Mei, 2024 na kukamilika tarehe 24 Mei, 2024.
Bwana Bulenga ameeleza kuwa Mkoa wa Mara una jumla ya Shule za Sekondari 28 zenye watahiniwa wa Kidato cha Sita kwa mwaka 2024 kutoka mikondo 102 na na wanafunzi kutoka mikondo 15 ya Vyuo vya Ualimu vitatu vilivyopo katika Mkoa wa Mara.
Bwana Bulenga ameeleza kuwa tayari Mkoa umepokea vifaa vyote na semina za wasimamizi wa mitihani zimefanyika kwa wasimamizi 312 ambao watahusika katika kusimamia mtihani huo katika Shule za Sekondari na Vyuo vya Ualimu vilivyopo katika Mkoa wa Mara.
Vyuo vya ualimu vilivyopo katika Mkoa wa Mara ni Chuo cha Ualimu Bunda (Wilaya ya Bunda), Chuo cha Ualimu Tarime (Wilaya ya Tarime) na Chuo cha Musoma Utalii (Wilaya ya Butiama) ambacho pia kinafundisha mafunzo ya ualimu.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa