Jumla ya wanafunzi 62,214 wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba wa mwaka 2024 katika Shule za Msingi 876 ambazo zitakuwa vituo vya mitihani zilizopo katika Mkoa wa Mara kuanzia kesho tarehe 11 hadi 12 Septemba, 2024.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Makwasa Bulenga amesema kati ya wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani, wavulana ni 29,424 na wasichana ni 32,790.
“Wanafunzi hawa ni wale walioandikishwa kuanza Darasa la Kwanza mwaka 2018 ambao kwa sasa wamekamilisha mzunguko wao wa elimu wa miaka saba mwaka 2024” amesema Bwana Bulenga.
Bwana Bulenga amesema mtihani wa wanafunzi hao unatarajiwa kufanyika katika vyumba vya mitihani (mikondo) 2,756 katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara.
Bwana Bulenga amesema maandalizi ya ufanyikaji wa mitihani huo katika Mkoa wa Mara yamekamilika ikiwemo semina kwa wasimamizi wa mitihani na usambazaji wa vifaa vya mitihani umeshafanyika na mpaka sasa hakuna mapungufu yaliyojitokeza.
Bwana Bulenga amesema kwa mwaka huu, Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA) limefanya maboresho katika mtihani huo ambapo tofauti na miaka mingine, mtihani wa mwaka huu utajibiwa katika karatasi ya maswali.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa