Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe.Dkt. Charles Mlingwa akitoa hotuba ya Ufunguzi wa kikao cha kujadili namna bora ya kukusanya Takwimu za UKimwi. Baadhi ya mambo muhimu aliyoyazungumza Mkuu wa Mkoa ni Pamoja na:
1. Umuhimu wa kutumia Takwimu katika kupanga mipango yetu ya Maendeleo.
2. Kuwa waadilifu katika kukusanya Takwimu za Ukweli ili kupata taarifa sahihi.
3. Kuhakikisha tunakuwa na afya njema maana ndio mwanzo wa kuweza kujiletea maendeleo maana bila afya hakuna maendeleo.
Katika kusisitiza hayo yote Mkuu wa Mkoa aliomba kila mshiriki kuweza kufuatilia mjadala huo kwa umakini na kutoa ushirikiano wa juu kwa timu zitakazoenda kwenye Halmashauri zao kukusanya Takwimu juu ya Ugonjwa wa UKIMWI. Kila mtendaji wa Serikali akiwajibika sehemu yake ya kazi basi tutaweza kupanga mipango sahihi ya maendeleo kwa kutumai Takwimu sahihi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa