Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde leo (Juni 21, 2024) amefanya ziara katika Wilaya ya Serengeti na kuwataka walimu wa darasa la kwanza na darasa la pili kutumia mbinu shirikishi katika ufundishaji wa wanafunzi.
Akizungumza katika kikao kazi na wasimamizi wa elimu Wilaya ya Serengeti ambapo amewasistiza walimu kuepuka kufundisha kwa mazoea hasa kwa darasa la kwanza na la pili kwa shule za msingi na Kidato cha kwanza.
“Mbinu shirikishi zikitumika kwa wanafunzi wa madarasa ya chini zitaleta ufanisi na matokeo chanya wakati watoto wanapoendelea na masomo yao katika ngazi za juu” amesema Dkt. Msonde.
Aidha, Dkt. Msonde amewataka walimu wanaofundisha somo la kiingereza shule za msingi kuongeza bidii na maarifa katika ufundishaji wa somo hilo kwani linachangamoto kutokana na wanafunzi wengi wamekuwa wakikaririshwa maneno magumu ya kiingereza bila kuelewa kile walichokariri.
Dkt. Msonde amewataka walimu kuwaandaa watoto kuanzia katika madarasa ya awali, darasa la kwanza, la pili na la tatu kwani kwa kufanya hivyo kutamjengea mtoto msingi mzuri tangu akiwa katika madarasa ya chini.
Kikao kazi hicho kilihudhuriwa na Maafisa Elimu kutoka ngazi ya Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.
Dkt. Msonde kesho anatarajiwa kuendelea na ziara yake katika Wilaya ya Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa