Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Boniface Simbachawene leo tarehe 2 Oktoba, 2024 amefanya ziara katika Wilaya ya Rorya na kutembelea, kukagua kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya maendeleo.
Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni mradi wa ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Rorya ambao utakapokamilika utakuwa na thamani ya shilingi bilioni 1.25 ambao umewekewa jile la msingi na mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ingri yenye thamani ya shilingi milioni 540 ambayo imezinduliwa.
Kabla ya kutembelea miradi hiyo, Mhe. Simbachawene ametembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rorya na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya ambapo alifanya kikao cha ndani na kusomewa taarifa ya Wilaya.
Akizungumza katika mradi wa shule ya Sekondari ya Ingri, Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe. Dkt. Khalfany Haule amesema kabla ya ujenzi wa shule hiyo, wanafunzi walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 12 kwenda shule na kurudi katika shule ya Serikali iliyokuwepo eneo hilo.
Mhe. Haule amesema shule hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 540 ujenzi wake umekamilika na tayari imesajiriwa na kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia Januari, 2024 na kwa sasa ina wanafunzi 120.
Akitoa taarifa ya shule hiyo, fedha za ujenzi wa shule hiyo zilipokelewa mwaka 2022/2023 jumla ya shilingi 584,228,028.00 na mradi huo ulitekelezwa kwa njia ya force account na kusimamiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa majengo yaliyojengwa mpaka sasa ni vyumba vya madarasa 8, ofizi za walimu 2, vyumba vitatu vya maabara, chumba cha Tehama, jengo la utawala, maktaba na matundu 12 ya vyoo vya wanafunzi.
Taarifa imeonyesha kuwa kukamilika kwa mradi huu kumesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Mirare ambapo awali wanafunzi wa eneo hilo waliokuwa wanasoma.
Akitoa taarifa ya mradi wa ukumbi, Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhandisi, Mhandisi Ramadhani Mcharo amesema Halmashauri imepokea shilingi milioni 750 ambazo imetumia kutekeleza mradi huo na kwa sasa ujenzi wa ukumbi huo umefikia asilimia 93.
Mhandisi Mcharo amesema ujenzi wa mradi huo umesaidia kuwezesha vikao vya madiwani kufanyika katika ukumbi huo pamoja na shughuli nyingine za Serikali.
Mhandisi Mcharo amesema kwa sasa Halmashauri inasubiria fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa shughuli zilizobakia ikiwa ni pamoja na ufitishaji wa top za milango, handrails katika ngazi, kumwaga jamvi, mfumo wa umeme awamu ya pili, Tehama, sauti, mfumo wa maji awamu ya pili, na uwekaji wa samani katika jengo hilo.
Baada ya ukaguzi wa miradi Mhe. Simbachawene alifanya mkutano wa hadhara katika eneo la utegi na baada ya hapo alielekea Tarime kuendelea na ziara yake.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa