Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Mhe. Mtanda alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.
Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Mhe. Mtanda ni mwanasiasa mzoefu na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi (Rukwa), Arusha (Arusha) na Urambo (Tabora).
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Mhe. Mtanda anatarajiwa kuapishwa rasmi leo tarehe 24 Mei, 2023 Chamwino, Dodoma.
Aidha, Mhe. Rais amemhamisha Mhe. Queen Cuthbert Sendiga aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Mhe. Charles Makongoro Nyerere aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Wakati huo huo, Rais amemteua Mhe. Kenani Kihongozi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora anachukua nafasi ya Mhe. Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko ya uhamisho na uteuzi huo unaanza mara moja.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa