• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mtambi awataka viongozi wa dini kuwahamasisha wananchi kuilinda Tanzania

Posted on: December 1st, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 01 Disemba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini wa Mkoa wa Mara katika ukumbi wa uwekezaji na amewataka kuwahamasisha waumini wao kuipenda na kuilinda Tanzania.

Mhe. Mtambi ambaye katika kikao hicho ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara amenukuu kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhusiana na jukumu la wananchi kuilinda nchi yao.

“Majeshi na vyombo vya usalama vipo kwa ajili ya kupata wataalamu na viongozi wa kuliongoza vyombo vya usalama lakini jukumu la ulinzi wa Tanzania ni la wananchi wote” amesema Mhe. Mtambi na kuwataka viongozi wa dini kuwakumbusha waumini wao kuhusiana na jukumu lao hili la kikatiba.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa dini kuwahamasisha waumini na jamii kwa ujumla kuilinda miundombinu ya umma, Serikali, taasisi na watu binafsi katika Mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla dhidi ya uharibifu wowote unaopangwa na watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania na kuwataka kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuhakikisha Tanzania inakuwa salama salama wakati wote.

Kanali Mtambi amewataka viongozi wa dini kuiweka Tanzania katika maombi wakati wote huku wakiendelea kuhubiri amani, umoja, upendo na mshikamano wa Watanzania kwa nyakati zote  na kuwataka kutokuruhusu hali ya kisiasa iliyopo kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini na kijinsia.

Mhe. Mtambi amewataka wananchi kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kufafanua kuwa pamoja na mitandao hiyo kuwa na manufaa makubwa, viongozi wa dini wanaowajibu wa kuwapa elimu wananchi kuhusu kuwa makini katika matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuwa makini na mambo wanayokutana katika mitandao ya kijamii.

Mhe. Mtambi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara amewahakikishia wananchi kuwa kamati hiyo ipo imara na tayari kuhakikisha Mkoa wa Mara unakuwa salama wakati wote.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Amani na Maridhino Mkoa wa Mara Shehe Ibrahim Msabaha amewataka viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika kuisemea amani nchi ya Tanzania na kuwataka viongozi wa dini kutoa taarifa wanapoona dalili zozote za uvunjifu wa amani.

Shehe msabaha amewataka viongozi hao kuacha kuegemea upande wowote wa siasa wakati huu Nchi inapokuwa katika hatari ya kuingia kwenye vurugu na badala yake amewataka viongozi hao kuwa imara katika kuhubiri amani, umoja, upendo na mshikamano wa Watanzania.

Shehe Msabaha ambaye pia ni Shehe Mkuu wa Mkoa wa Mara amesema Mkoa wa Mara unatekeleza maagizo ya Mufti Mkuu wa Tanzania kuhusiana na kusali Kanuti wakati huu ili watu wote wenye nia ovu na amani ya Tanzania waweze kuadhibiwa na hiyo Kanuti.  

Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Amani na Maridhiano Mkoa wa Mara Shehe Juma Masiroli amewataka viongozi wa dini kuzungumza na waumini wao kuhusu umuhimu wa kulinda amani katika maeneo yao.

Shehe Masiroli amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa kwa kuanzisha utaratibu wa kukutana na viongozi wa dini kila mwezi jambo ambalo amesema limeimarisha mahusiano kati ya viongozi wa dini na Serikali.

Kikao cha Kamati ya Usalama na viongozi wa dini ni mwendelezo wa vikao vya kawaida vya Mkuu wa Mkoa wa Mara kukutana na makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo viongozi wa dini wa Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mtambi awataka viongozi wa dini kuwahamasisha wananchi kuilinda Tanzania

    December 01, 2025
  • Kusaya aridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mara

    November 27, 2025
  • Kusaya aongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi

    November 26, 2025
  • Mtambi awataka wakandarasi Mara kutekeleza miradi usiku na mchana

    November 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa