• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

Posted on: August 22nd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 22 Agosti, 2025 amekutana na kuzungumza na viongozi wa dini wa Mkoa wa Mara waliokuwa wanaendelea na kikao chao katika Ukumbi wa Uwekezaji na kuwataka kuendelea kuhubiri amani ili uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ufanyike kwa amani na utulivu.

Akizungumza katika kikao hicho cha viongozi wa Kamati ya Amani na Kamati ya Amani na Maridhiano, Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa dini kuwaongoza waumini wao kumtanguliza Mungu katika mambo yote wanayoyafanya wakati huu wa uchaguzi ili Tanzania iweze kuvuka salama ikiwa katika umoja, amani na mshikamano.

“Muwahimize waumuni watambue kuwa bila ya kumtanguliza Mwenyezi Mungu utandawazi na wanasiasa wasio na nia nzuri na Taifa letu wanaweza kutuvuruga kwa kutumia mitandao ya kijamii, lakini tukimtanguliza Mungu tutakuwa na umoja na mshikamano wetu” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewashukuru viongozi wa dini kwa namna walivyotoa ushirikiano katika uchaguzi wa Sreikali za mitaa wa mwaka 2024 na kuongeza kuwa katika Mkoa wa Mara kulikuwa kupanuka kwa demokrasia na ukomavu wa kisiasa ambao uliwezesha uchaguzi kulifanyika kwa amani na utulivu.

“Ninawaomba tushirikiane ili tufanye vizuri katika uchaguzi huu kuliko mwaka jana, ili wananchi wetu waendelee kupambana kujenga uchumi wao kwani hawawezi kujenga uchumi kama hamna amani na utulivu” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa dini kuwakumbusha waumini wao kuwa maisha yataendelea baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuwataka kuwahamasisha waumuni kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi na kwa wale wenye sifa kupiga kura ili kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Mhe. Mtambi amewashukuru viongozi hao kwa kuandaa kikao hicho ili kuweza kujadiliana mambo muhimu kwa mwaka huu wa uchaguzi ili uchaguzi ufanyike katika hali ya amani na utulivu na kuwataka kuendelea kuitisha vikao hivyo ili kupeana hamasa ya kulinda amani.

Kanali Mtambi amewapongeza viongozi wa dini kwa kazi kubwa ya kuilea jamii wanayoifanya hapa nchini na kuongeza kuwa jamii isiyokuwa na hofu ya Mungu inakuwa ni jamii hatari sana na kuwashukuru kwa jinsi wanavyoilea jamii ya Kitanzania kwa kuhubiri amani, upendo na msihakamo.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara umejipanga kuhakikisha mambo yanayotokea katika Mataifa yanayouzunguka Mkoa hayaharibu amani, umoja na mshikamano wa wananchi kwa kuwa tunu hizo zimejengwa katika mizizi mirefu ambayo Watanzania kwa umoja wao wanaiamini.  

“Sisi Watanzania tunakaa pamoja tunazungumza na tunapanga mambo yetu, tunasonga mbele, hatuwezi kuiga mambo ambayo hayana maana kutoka kwa majirani zetu” na kuongeza kuwa hata jamii ikitamani kuiga, viongozi wa dini wawakemee.

Aidha, Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa dini kulisaidia Taifa kulea kizazi cha sasa hivi kukirudhisha katika hofu ya Mungu na kukiongoza katika maisha bora yanayojali utu wa watu na kutoa kipaumbele katika amani na utulivu wa Mkoa wa Mara na Nchi ya Tanzania.

Kwa upande wake, Katibu wa Kamati ya Amani na Maridhiano Sheikh Juma Masiroli amesema mwaka 2025 nchi inaingia kwenye uchaguzi mkuu, viongozi wa dini kwa umoja wao waende kwenye nyumba za ibada wazungumze na waumini wao na kuliombea Taifa ili nchi ivuke salama.

Sheikh Masiroli amesema kama Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Mara wanavyoishi kwa umoja na mshikamano wakati wote, ndivyo viongozi hao wanavyopaswa kuwaongoza pia waumini wao katika amani na utulivu wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi.

Sheikh Masiroli amewashukuru viongozi walioshiriki na kuzungumza kuhusu amani na utulivu wa Mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla na kuwataka kuendelea kuiombea nchi na viongozi wote wa Nchi hii ili amani iliyopo iendelee kutawala.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Amani na Maridhiano Askofu Jacob Rutubinga amewataka viongozi wa dini kuhakikisha kuwa Mkoa wa Mara unaongoza kwa amani na utulivu wakati wote wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na mikoa mingine ije kujifunza namna ya kulinda amani na utulivu wakati wa uchaguzi.

Mchungaji Rutubinga amewashukuru viongozi hao kwa kuimarisha umoja baina yao ambao amesema unaendelea kuimarika kutokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa dini zote.

Amewataka viongozi hao kuendelea na umoja huo ambao amesema ni jambo zuri na linalosaidia kuwafundisha waumini wao namna ya kuishi pamoja katika jamii bila kuangalia tofauti za Imani, itikadi za kisiasa na kipato.

Mchungaji Rutubinga amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa ushirikiano anaoutoa kwa viongozi wa dini wa Mkoa wa Mara na kuongeza kuwa viongozi hao wanaouombea Mkoa ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu na wanamuombea

Kwa upande wake, Shehe wa Mkoa wa Mara Shehe Msabaha Kassimu amesema kila mtu anatakiwa kuilinda amani na utulivu uliopo, huu ni Mkoa ni wa amani na wananchi wake wanajua ustaarabu na ni wakarimu bali hawapendi kuonewa wala kumwonea mtu na wamekuwa wakitafsiriwa vibaya na watu ambao hawawafahamu.

Shehe Msabaha amewataka viongozi wa dini kuwahimiza waumini kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali kuhusu mambo mbalimbali kwani maelekezo hayo yanaumuhimu mkubwa kwao.

Kwa upande wake, Mchungaji Ibrahim Sasi amesema kuwa jukumu kuu la viongozi wa dini ni  kusababisha amani na utulivu kwa kuwaongoza waumini katika kumtumainia Mungu katika kipindi hiki.

“Sisi tusijihusishe na mambo yanayoweza kusababisha amani kukosekana, tumeitwa kumtumikia Mungu  tusiwe sababu ya kusababisha uvunjifu wa amani, na viongozi wa dini tuwe mfano mwema katika jamii yetu” amesema Mchungaji Sasi.

Kwa upande wake Padri Julius Auko Ogolla, Naibu Askofu Jimbo Katoliki Musoma amesema viongozi wa dini kwa wanakoelekea wanahitaji maombi na kuwasaidia waumini kuelezea umuhimu wa nchi kuwa na amani na utulivu.

Padri Ogolla amesema Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limeelekeza Kanisa kufanya mafungo ya saa 24 kuanzia tarehe 22-25 Agosti, 2025 kwa ajili ya sala za kuombea amani, uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na watu walioko Tanzania wawe na amani na hivyo makanisa na majimbo yote ya Tanzania yatashiriki sala hiyo.  

Padri Ogolla amewataka viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kutambua kuwa hii ni nchi yao na wamelelewa katika amani na wasitumie uchaguzi kuanzisha fujo bali waendelee kuiombea ili kila mmoja aingie akiwa na amani ili wapatikane viongozi wanaostahili.

Viongozi mbalimbali walioshiriki kikao hicho wameafiki kuandaa ibada ya pamoja kwa ajili ya kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili uweze kufanyika kwa amani na utulivu.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

    August 22, 2025
  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • Mwenge wakagua miradi ya bilioni 6 Musoma

    August 18, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa