• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mara ampokea DC Bunda

Posted on: February 27th, 2025

Adeladius Makwega-Musoma MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amempokea rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyoge aliyefika kurepoti leo baada ya kuhamishiwa akitokea Wilaya ya Maswa na kumtaka kusimamia amani na utulivu na hususan mwaka huu wa uchaguzi Mkuu.

Mhe. Mtambi amesema wakati wa uchaguzi wako baadhi ya watu wanapenda kuanzisha chochochoko na kuongeza kuwa Mkoa wa Mara hautaruhusu mtu yoyote aichezee amani na utulivu uliopo kwa sasa.

“Shabaha yetu ni kujenga uchumi wa Mkoa na hususan kwa ajili ya wananchi wanaoishi katika Mkoa wa Mara ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika Mkoa na hayo yatafanikiwa tu endapo amani na utulivu vitaendelea kutawala” amesema Mhe. Mtambi. 

Mhe. Mtambi amewataka Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kuwa makini na  homa za kisiasa zinazoweza kuvuruga amani na utulivu uliopo na kuutoa Mkoa kwenye adhma yake ya kukuza uchumi wa wananchi wake.

Kanali Mtambi amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi wapo salama na wanaendelea kufanya shughuli zao kama kawaida na wanasiasa wanafanya siasa zao kama kawaida kwa amani na utulivu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo ya Serikali. 

“Pale Bunda Mji tuna madini na wananchi wapo kazini wakichimba madini yaliyogundulika katika eneo hilo na wajibu wetu kama Serikali ni kuwawekea mazingira wachimbaji hao wadogo waweze kufanya shughuli zao na kulipa kodi zinazohitajika kwa Serikali” amesema Mhe. Mtambi.

Akizungumza katika mapokezi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Kaminyoge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini.

Mhe. Kaminyonge amesema atatekeleza maagizo aliyompatia kwa nguvu na moyo wote na kuwaomba wananchi wa Wilaya ya Bunda wampokea na kumpatia ushirikiano.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vincent Naano Anney amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi kwa kufanya naye kazi vizuri kwa kipindi chote akiwa Bunda na kuahidi kufanya kazi kwa vizuri akiwa Maswa kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi afungua kambi ya madaktari bingwa na bobezi 64 Mara

    June 23, 2025
  • Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara wapatiwa mafunzo

    June 20, 2025
  • Mara mshindi wa pili UMITASHUMTA 2025

    June 18, 2025
  • Zingatieni miongozo ya kilimo cha tumbaku- Dkt. Haule

    June 18, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa