Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi leo tarehe 19 Aprili 2022 amezindua rasmi Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Akizundua Bodi hiyo, Mheshimiwa Hapi amewataka wajumbe wa bodi hiyo kuwatendea haki wananchi kwa kutoa ushauri mzuri kuhusiana na usimamizi na uendeshaji wa hospitali hiyo kwa Menejimenti ya Hospitali na kwa Serikali.
“Katika hospitali zetu, kuna tatizo la udhibiti mbovu wa dawa na hivyo kusababisha wizi wa dawa katika hospitali nyingi za umma, ninaomba mkalisimamie ili lisitokee katika Mkoa wa Mara na kama lilikuwepo basi liwe historia” alisema Mheshimiwa Hapi.
Aidha ameitaka bodi hiyo kusimamia mapato na matumizi ya Hospitali hiyo na kuhakikisha kuwa mapato yote yanakusanywa kupitia mfumo wa mapato ya hospitali (GoTHOMIS) wakati wote wa kutoa huduma za hospitali.
Mheshimiwa Hapi ameagiza bodi hiyo kusimamia ujenzi unaoendelea katika hospitali hiyo ili ukamilike na hospitali hiyo iweze kuhamia katika eneo la Kwangwa.
Mkuu wa Mkoa ameiahidi bodi hiyo ushirikiano kutoka kwa viongozi wote wa Mkoa wa Mara katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma, Michael Msoganzila amewataka wajumbe kushirikiana katika kutimiza majukumu ya bodi hiyo.
Bwana Mloganzila amewapongeza wajumbe wapya kwa kuteuliwa na wale waliomaliza muda wao kwa kazi nzuri waliyoifanya wakati wote wakiwa wajumbe wa bodi hiyo.
Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ina wajumbe 11 ambao wanatoka katika taasisi mbalimbali na wenye utaalamu mbalimbali na wanaoteuliwa kwa muda wa miaka mitatu mitatu.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa