• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

Posted on: October 13th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evance Alfred Mtambi leo tarehe 13 Oktoba, 2025 amewapokea  madaktari bingwa na bobezi maarufu kama Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 waliofika Mkoa wa Mara kuanza kambi maalum ya madaktari wa Mama Samia watakaotoa huduma katika Hospitali za Halmashauri za Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya afya unaoruhusu kuanzishwa kwa programu ya kuwapelekea madaktari bingwa katika Hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya.

“Mhe. Rais amefanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya msingi katika vituo vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Mara jambo ambalo linawezesha madaktari bingwa kufanyakazi vizuri katika vituo hivyo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema huduma za kibingwa na kibobezi zinaposogezwa jirani na wananchi zinasaidia kuokoa muda na fedha za wananchi kwa ajili ya usafiri, kuokoa maisha na kuzuia ulemavu kwa wagonjwa na kuongeza mapato ya Halmashauri husika.

“Wagonjwa wengi wanapoteza maisha wakiwa njiani kuelekea hospitali kubwa kwa ajili ya kupata matibabu ya kibingwa na Mhe. Rais kaliona hili na kuamua kuwaleta madaktari bingwa na bobezi ndani ya kilometa 30 ili kuokoa maisha” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema katika awamu tatu zilizopita kambi za madaktari bingwa zimefanyika kwa mafanikio makubwa na kuwasistiza Waganga Wakuu wa Halmashauri kusimamia utoaji wa huduma, ukusanyaji wa mapato na kuwasilisha taarifa kila siku Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kuhusiana na utekelezaji wa zoezi hilo.

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni za uchaguzi zinazoendelea na kupiga kura tarehe 29 Oktoba, 2025.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya amewakaribisha madaktari hao Mkoa wa Mara na kuwahakikishia mazingira mazuri ya kufanyiakazi na upatikanaji wa vitendea kazi.

Ndugu Kusaya amewataka madaktari bingwa na bobezi wanaohitaji kubaki katika Mkoa wa Mara kumtaarifu ili taratibu za kuwahamisha ziweze kufanyika.  

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Zabron Masatu amesema hii ni awamu ya nne madaktari bingwa na bobezi wanapolelewa katika Mkoa wa Mara kuanzia Juni, 2026 na mpaka sasa takriban wagonjwa 6,000 wameonwa na madaktari hao.

Dkt. Masatu amesema madaktari hao watawaona wagonjwa wenye changamoto mbalimbali na kufanya upasuaji pale unapohitajika na kati ya wataalamu hao kila kituo kitakachofikiwa kitapata madaktari bingwa watano wa magonjwa mbalimbali na muunguzi mbobezi mmoja.

Kwa upande wake Mratibu wa Kambi ya madaktari Bingwa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Grace Mariki amesema katika awamu hii, Wizara ya Afya imeleta madaktari bingwa na bobezi 64 na watafanyakazi kuanzia leo tarehe 13 hadi 17 Oktoba, 2025 katika Hospitali zote za Halmashauri za Mkoa wa Mara na kituo cha Afya Ikizu na Kasahunga katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Dkt. Mariki amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Mara kuchangamkia fursa hiyo adhimu na kupata huduma za matibabu za kibingwa na bobezi karibu na maeneo yao.

Hafla ya mapokezi hayo imefanyika katika ukumbi wa uwekezaji na kuhudhuriwa pia na Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Maafisa kutoka Wizara ya Afya na Timu ya Usimamizi wa Sekta ya Afya katika Mkoa wa Mara na Waganga Wakuu wa Halmashauri.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

    October 03, 2025
  • Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa