Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ofisini kwake amempokea na kuzungumza na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala ambaye amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Mara.
Akizungumza baada ya kuwasili, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amempongeza Mhe. Mtambi kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuuongoza Mkoa wa Mara.
Kamishna Makakala ameeleza kuwa lengo la ziara yake katika Mkoa wa Mara ni kushughulikia maombi ya walowezi wa muda mrefu ambao walihamia kutoka nchi ya Kenya ambao wanadai vitambulisho vya uraia.
“Tunashughulikia vitambulisho hivyo ili tunapoelekea kwenye uchaguzi wale wanaostahili kupata vitambulisho hivyo wawe navyo ili iwasaidie katika kutumia haki yao ya kuchagua viongozi” amesema Dkt. Makakala.
Dkt. Makakala amesema ofisi yake inashughulikia changamoto za ofisi ya Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Mara ikiwemo suala la upungufu wa watumishi na usafiri kwa maafisa wa uhamiaji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amemshukuru Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kwa kufanya ziara katika Mkoa wa Mara na kumshukuru kwa ushirikiano wa ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mara kwa viongozi wa Mkoa.
Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara una waloweze wengi ambao wamekuwa wakifuatilia kadi ya mpiga kura, namba ya utambulisho wa Taifa na vitambulisho vingine vya uraia na wamekuwa wakiwatumia wanasiasa kufuatilia vitambulisho hivyo.
Mhe. Mtambi amemuomba Dkt. Makakala asiondoke kabla ya kuonja nyama choma ya Mkoa wa Mara na kutokana na mifugo yake kufugwa kwenye mazingira mazuri na kujionea utamu na ubora wa nyama choma ya Mkoa wa Mara.
“Haya mazingira inaonekana Mungu aliyaandaa kwa ajili ya wanyama na ndio maana sehemu kubw aya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ipo Mkoa wa Mara bahati mbaya wanyama hawa hawauzwi sana Tanzania wanapelekwa nchi jirani kwa njia ya magendo” amesema Mhe. Mtambi.
Katika ziara hiyo, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji ameambatana na Maafisa mbalimbali kutoka Jeshi la Uhamiaji Makao Makuu na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa