Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee leo ameanza ziara ya kikazi katika Wilaya ya Musoma na Wilaya ya Butiama kwa kutembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara kwa lengo la kujitambulisha.
Akizungumza baada ya kujitambulisha na kukaribishwa, Mkuu wa Mkoa amewaahidi ushirikiano yeye mwenyewe na viongozi wote wa serikali wa Mkoa wa Mara.
“Mimi ninawaahidi tutatoa ushirikiano wa kutosha kwa Chama cha Mapinduzi na viongozi wa Chama na niwaombe ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi” ameeleza Mheshimiwa Mzee.
Mheshimiwa Mzee ameeleza kuwa anaamini katika mabadiliko ya kimaendeleo na ubunifu kwa ajili ya kuutoa Mkoa wa Mara sehemu ilipofikia kwenda katika maendeleo zaidi.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Bwana Lengaeli Akyoo amemkaribisha Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa watu wa Mkoa wa Mara wamefurahia uteuzi wao na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi hao.
Aidha, amewapongeza kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mheshimiwa Rais na kuwakaribisha Mkoa wa Mara na hususan katika Chama cha Mapinduzi.
katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu ambaye pia amewasili Mkoa wa Mara tarehe 5 Agosti, 2022 baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 28 Julai, 2022.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Mzee katika Mkoa wa Mara baada ya kuwasili tarehe 6 Agosti, 2022 baada ya kuteuliwa na Rais tarehe 31 Julai, 2022 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa