RC AFANYA ZIARA WILAYA YA RORYA
Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee leo tarehe 11 Agosti, 2022 amefanya ziara ya kujitambulisha katika Wilaya ya Rorya.
Mheshimiwa Mzee alipokewewa na wenyeji wake na baada ya hapo alitembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Rorya na kuwasalimia wananchi wa Rorya katika eneo la Mika.
Baadaye, Mkuu wa Mkoa wa Mara ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya na kumwelekeza Katibu Tawala wa Wilaya ya Rorya kufanya ukarabati mdogo mdogo wa jengo hilo wakati tunasubiria bajeti ya serikali kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa jengo hilo.
Ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya na kuagiza marekebisho mbalimbali katika nyumba ya watumishi (three in one) inayojengwa katika eneo hilo.
Marekebisho hayo ni pamoja na uwekaji wa ngazi nyuma ya nyumba hiyo, vigae vya chooni, ukuta na uwekaji wa PVC kwenye nyumba hiyo.
Mkuu wa Mkoa pia ametembelea ofisi za Polisi Wanamaji katika eneo la Suba na kujionea boti ya doria ambayo inatumia mafuta mengi kutokana na kuwa na injini kubwa ya cc 4000 badala ya cc 40 inayohitajika.
Aidha, Mheshimiwa Mzee alitembelea kipenyo cha mpaka wa Tanzania na Kenya katika eneo la Kilongwe Wilayani Rorya na kutaarifiwa kuwa kipenyo hicho kinakusanya wastani wa 300,000 kwa mwezi.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mzee aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu, viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Rorya.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa