Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mzee leo tarehe 17 Agosti, 2022 ametembelea katika wilaya ya Bunda katika mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha.
Akiwa Bunda, ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Bunda kuhakikisha kuwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji inayoanza kujengwa sasa isimamiwe vizuri kwa kufuata matakwa ya kiuhandisi na kwa ubora ili iweze kuwa ya mfano.
“Ninataka hospitali hii niifuatilie, ikidhi matakwa yote ya kiuhandisi na ubora na ikamilike kwa wakati ili tupate miradi ya mfano katika Mkoa wa Mara” alisema Mheshimiwa Mzee.
Aidha, Mheshimiwa Mzee ameaigiza Halmshauri ya Mji wa Bunda kupanda miti kulingana na mpango wa matumizi ya ardhi wa eneo hilo, kusawazisha eneo hilo na kuhakikisha mahitaji yote ya kiutaalamu ya eneo la ujenzi yapo.
Mheshimiwa Mzee amewaagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Mji wa Bunda kufuatilia hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwana Emmanuel Mkongo ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza Juni, 2022 hata hivyo baadaye waligundua tofali zilikuwa chini ya kiwango na kuanza ujenzi upya.
Bwana Mkongo ameeleza kuwa ujenzi huo umepangwa kukamilishwa ndani ya miezi minne na kwa sasa vifaa vyote vya ujenzi wa mradi huo vimeshanunuliwa.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Bwana Msalika Robert Makungu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya Dkt. Juma Mfanga, viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bund ana Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa