Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 24 Mei, 2023.
Uapisho huo umefuatia Rais kumteua Mhe. Mtanda tarehe 23 Mei, 2023 kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Mhe. Mtanda ni mwanasiasa mzoefu na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi (Rukwa), Arusha (Arusha) na Urambo (Tabora).
Mhe. Mtanda anatarajiwa kuwasili Mkoa wa Mara tarehe 25 Mei, 2023 kuanza kutekeleza majukumu yake katika Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa