Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Adam Kighoma Malima amezindua rasmi msimu wa ununuzi wa zao la pamba Mkoa wa Mara. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika kijiji cha Bukore wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara siku ya tarehe 08 Mei, 2018.
Akizungumza na wakulima wa pamba, wanunuzi wa pamba,mameneja wa banki za CRDB na NMB pamoja na viongozi wa vyama vya ushirika Mkuu wa Mkoa alisitiza mambo mbalimbali ili kuhakikisha msimu wa mauzo hautawakatisha tamaa wakulima wa pamba. Malima alisema ni lazima vyama vya ushirika vyote pamoja na wakulima wawe na akaunti za banki kwa kuwa mauzo hayatafanyika kwa njia nyingine yeyote isipokuwa benki ili kuepuka kudhulumiwa kwa wakulima. Serikali imefanya kila jitihada kuhakikisha mkulima wa zao la pamba hatajuta kwanini alilima pamba mwaka huu.
“Imekuwa ni tabia iliyozoelekwa kwa wanunuzi wa pamba kujipangia bei ya ununuzi ambayo inamnyonya mkulima.Katika msimu huu Serikali imetoa bei elekezi ya zao la pamba ambayo kwa kila Kg 1 ni shilingi 1,100/=. Vilevile Serikali imesamehe gharama zote za Viwatilifu ambavyo wakulima walikopeshwa kipindi cha kilimo.Hii itawawezesha ninyi wakulima kupata faida kubwa pindi mtakapouza pamba yenu. Nawaomba viongozi wa vyama vya ushirika muwe waadilifu kwa kuwa Serikali haitacheka na ninyi mkifanya vitendo vya kifisadi. Tunataka mkulima wa pamba abadili maisha yake kwa kuongeza kipato kutokana na mauzo ya pamba yake.Lakini pia wakulima mhakikishe manuza pamba yenye ubora ambayo hamjachanganya na mawe au maji ili mpate faida kubwa kwa kuwa hata wanunuzi hawapendi vitu visivyo na ubora mana na wao watapata hasara.” Alisema Malima.
Naye Afisa Kilimo wa Mkoa wa Mara Denis Nyakisinda, alisema kwa mwaka huu wa kilimo Mkoa wa Mara umelima jumla ya hekta 70324.5 za pamba ambalo ni ongezeko la asilimia 26.5 ukilinganisha na mwaka 2016/2017 ambapo jumla ya hekta 52,423 tu ndizo zililimwa pamba. Mkoa unatarajia kuvuna tani 60,000 za pamba msimu huu wa pamba.Katika msimu huu makampuni makubwa mawili ya Olam na SMC yameingia mkataba na Halmashauri ya Bunda kuhakikisha pamba yote ya wakulima inanunuliwa na hakuna mkulima atakayerudi na pamba yake bila kuiuza. ‘’Sisi kama Mkoa tutaendelea kushirikiana na wakulima hawa na kuwapa msaada wa kitaalamu ili kuhakikisha kilimo cha pamba kinaleta tija kwao na Serikali kwa ujumla ili kuongeza kipato cha mkulima na kuendana na Sera ya Tanzania ya Viwanda.Soko la pamba lipo limeni kwa wingi wakulima” Alisema Nyakisinda.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi Lidya Bupilipili alishukuru jitihada kubwa inayofanywa na Mkuu wa Mkoa za kuhakikisha maelekezo
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa