Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara na kuitaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kutenga bajeti maalum kwa ajili ya kuweka alama maalum ya kuutambulisha Mkoa wa Mara.
Mhe. Mtanda ametoa maelekezo hayo katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kuiagiza TANROADS kuweka alama hizo hata katika ngazi ya Wilaya kwa ajili ya kutangaza shughuli kuu za wilaya hizo.
“Tunatakiwa kuwa kama Mikoa mingine, tunatarajia kupokea wageni wengi wanaokuja kwa ajili ya utalii mara baada ya kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Musoma, hivyo lazima tuwe na alama itakayoutambulisha Mkoa wetu wa Mara” amesema Mhe. Mtanda.
Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe ameeleza kuwa agizo hilo wamelichukua na watalifanyia kazi.
Mhandisi Maribe ameeleza kuwa katika bajeti ya mwaka 2024/2025 jumla ya shilingi 226,396,000,000 zimeombwa kutoka Mfuko wa Barabara na Serikali Kuu kwa ajili ya kugharimia ukarabati, ujenzi wa kiwango cha lami na usanifu wa barabara zenye urefu wa jumla ya kilomita 380.51 katika Mkoa wa Mara.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa mara ameeleza kuwa jumla ya shilingi 56,294,609,287.84 kimepangwa kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya vivuko.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa