Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Serengeti Nyama choma Utalii Festival itakayofanyika katika eneo la mnadani, katika Mji wa mugumu tarehe 01 Novemba, 2024.
Ratiba iliyotolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti Bibi Angelina Marco inaonyesha kuwa tamasha hilo litaanza saa 12.00 asubuhi kwa kufanya mazoezi ya kukimbia na baadaye washiriki watapata supu na kuanza mashindano ya michezo mbalimbali hadi mchana.
Bibi Marco amesema mashindano ya kuchoma nyama yatafanyika mchana na kuhitimishwa na burudani katika uwanja huo wa mnadani kutoka kwa wasanii mbalimbali kabla ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali watakaoshiriki katika tamasha hilo.
Tamasha hilo limedhaminiwa na wadau mbalimbali wa nyama choma na utalii ikiwemo Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL).
Serengeti Nyama Choma Festival ni moja ya matukio ya yaliyoandaliwa katika Mkoa wa Mara mahususi kwa ajili ya uhamasishaji wa wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024.
Kauli mbiu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ni “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa