• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi amtaka mkandarasi kukamilisha mradi kwa wakati

Posted on: February 17th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 17 Februari, 2025 ameshuhudia makabidhiano ya mradi wa uchimbaji wa visima saba vya kilimo cha umwagiliaji katika Mkoa wa Mara na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mhe. Mtambi ametoa maagizo hayo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika kijiji cha Kwikuba, Kata ya Busambara Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kumtaka mkandarasi huyo na wengine wote ndani ya Mkoa wa Mara kutekeleza miradi yao kwa wakati.

“Serikali imekupatia zabuni hii baada ya kujiridhisha na uwezo wa kampuni yenu, sasa Mkoa wa Mara hatutaki visingizio katika utekelezaji wa mradi huu kama kuna changamoto tutaarifiwe mapema ili kuweza kuitatua” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi anasema miradi ya maendeleo inalenga kutatua changamoto za wananchi  na kuwataka wakandarasi wote wa Mkoa wa Mara kujitahidi kukamilisha miradai yao kwa wakati ili iweze kutumika na kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Mara.

Kanali Mtambi amesema mradi huu unaleta mwanga kuelekea maisha bora kwa wananchi wa Mkoa wa Mara ambapo mkulima anajua kwa uhakika analima linin a atavuna lini mazao yao na hivyo kuleta uhakika wa chakula.

Mhe. Mtambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Halmashauri zilizopata visima hivyo kutafuta masoko ya uhakika ya mazao yatakayolimwa katika mashamba yenye visima hivyo ili kuwahamasisha wakulima zaidi kushiriki kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake, Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Mara Mhandisi Adelialidy Mwesiga amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Tume ya Taifa ya Uwagiliaji itachimba visima 1,300 nchi nzima katika awamu hii ya kwanza visima 70 vitachimbwa na kati ya hivyo visima saba vitachimbwa katika Mkoa wa Mara.

Mhandisi Mwesiga amesema katika Mkoa wa Mara visima hivyo vinategemewa kuchimbwa katika wilaya za Musoma, Bunda, Butiama na Tarime kisima kimoja kila Wilaya wakati katika Wilaya ya Serengeti vinatarajiwa kuchimbwa visima vitatu na visima hivyo vinatarajiwa kuwanufaisha wakulima zaidi ya 700 wa wilaya hizo.

“Katika Mkoa wa Mara mradi huu unategemewa kugharimu shilingi 244,033,440 na utatekelezwa na Mkandarasi mzawa na kusimamiwa na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uwagiliaji” amesema Mhandisi Mwesiga.

Mhandishi Mwesiga amesitaja shughuli zitakazofanyika kuwa ni pamoja na utafiti wa upatikanaji wa maji katika maeneo yote saba, uchimbaji wa visima, uhakiki wa kujua kiasi cha maji kilichopatikana na ufungaji wa mifumo ya umwagiliaji.

Bwana Mwesiga amesema mfumo wa miundombinu ya umwagiliaji utakaotumika ni umwagiliaji kwa njia ya matone na mazao yatakayolimwa ni mbogamboga na mahindi na eneo zaidi ya ekari 40 zitamwagiliwa na kisima kimoja.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa mradi huo Mubarak Twaha Ngwada wa Kampuni ya MNFM Construction amesema mradi huo wa kuchimba visima saba katika Mkoa wa Mara walitakiwa kukamilisha ndani ya miezi sita kwa mujibu wa mkataba wa zabuni yao iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uwagiliaji.

“Hata hivyo tunatarajia kuukamilisha mradi huu pamoja na kupima uwingi wa maji hayo ifikapo tarehe 4 Aprili, 2025 kwa visima vyote saba vya Mkoa wa Mara ili wananchi waendelee na shughuli za uzalishaji mali” ameahidi Bwana Ngwada.

Bwana Ngwada ameishukuru Serikali kwa kuiamini na kuipatia kampuni hiyo zabuni ya kutekeleza mradi huo na kuahidi kuutekeleza kwa ubora na ndani ya muda uliowekwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwikuba Bwana Kamunyilo Kubega Dominiko amesema tayari kijiji hicho kimepata eneo la kufanya kilimo cha umwagiliaji na kuunda kikundi cha wakulima wa kilimo cha umwagiliaji ambao watanufaika na mradi huo.

Bwana Dominiko amesema kwa kutumia maji ya kisima hicho wanakikundi wataweza kulima mazao mbalimbali ya muda mfupi ikiwemo mahindi na mbogamboga na kuboresha hali ya upatikanaji wa chakula katika eneo hilo.

Bwana Dominiko ameishukuru Serikali kwa kuleta mradi huo ambao amesema ni mkombozi wa wakulima wadogo wadogo wa kijiji hicho ambao awali walikuwa wanalima kwa kutegemea mvua na hawakuwa na uhakika wa kuvuna mazao yao.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC azitaka Wilaya kuongeza nguvu maandalizi ya Mwenge 2025

    May 09, 2025
  • Mtambi akabidhi tuzo na kinyago washindi wa Mwenge 2024

    May 09, 2025
  • Mtambi alitaka jukwaa la ushirika kuongeza ubunifu

    May 08, 2025
  • Jumuiya ya Waislamu Musoma yachangia madawati

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa