Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameongoza hafla fupi ya kukabidhi magari mawili yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mara yatakayotumika katika Wilaya za Tarime na Serengeti.
Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo, Mhe. Mtambi amewataka watendaji wa RUWASA waliokabidhiwa magari hayo kuhakikisha kuwa magari hayo yanatumika vizuri na yawawaongezea kasi ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
“Kwa sasa RUWASA Mkoa wa Mara mna jumla ya magari matano ukijumlisha na magari matatu yaliyokuwepo na pikipiki 35, ni matumaini yangu kuwa magari haya yatatumika kuboresha huduma za upatikanaji wa maji kwa wananchi” amesema Mhe. Mtambi.
Aidha, ameitaka Mhe. Mtambi amesema RUWASA imepanga kununua pikipiki 25 ili kuimarisha suala la usafiri kwa wataalamu katika kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Mara.
Kanali Mtambi amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia matumizi ya magari hayo ili yadumu kwa muda mrefu na yatumike kutoa huduma kwa wananchi wa Wilaya hizo.
Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mara Mhandisi Tulimpoki Mwakalukwa ameishukuru Serikali kwa kutoa magari hayo ambayo amesema walikuwa wanayahitaji sana kama kitendea kazi muhimu.
Mhandishi Mwakalukwa amesema tayari Serikali ilileta amagari mengine matatu ambayo yaligawiwa kwa Ofisi ya RUWASA Mkoa wa Mara, Wilaya ya Butiama na Wilaya ya Bunda wakati gari zilizokabidhiwa leo ni kwa ajili ya Wilaya ya Serengeti na Wilaya ya Tarime.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mwakalukwa, kwa sasa Wilaya ambazo hazina magari ni Musoma na Rorya ambayo yameshaombwa Serikalini.
Mhandisi Mwakalukwa amemshukuru Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso kwa kuidhinisha manunuzi na kuugawia Mkoa wa Mara magari hayo ambayo ameahidi kuyasimamia kwa ukaribu katika matumizi yake.
Kwa upande wake, Mhandisi wa RUWASA Wilaya ya Tarime Mhandisi Malando Mashapu ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa vitendea kazi muhimu kwa RUWASA Wilaya ya Tarime.
Mhandisi Mashepu ameahidi kuwa magari hayo yatawasaidia katika kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kuhakikisha wanapata maji na kutatua changamoto za maji kwa wakati.
Hafla ya kukabidhi magari hayo imehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, RUWASA na Halmashauri za Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa