• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aitaka Bunda DC kuwasilisha Mkakati wa kukusanya milioni 700

Posted on: June 13th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Evans Alfred Mtambi leo tarehe 13 Juni, 2025 ameshiriki kikao maalum cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kutoa hadi tarehe 16 Juni, 2025 Halmashauri iwasilishe mkakati wa kukusanya shilingi milioni 700 za mapato ya ndani kufikia Juni 30, 2025.

Mhe. Mtambi ametoa agizo hilo baada ya Halmashauri hiyo kukusanya shilingi bilioni 1.8 ya mapato ya ndani hadi tarehe 31 Mei, 2025 ambayo ni sawa na asilimia 75 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 2.5 katika mwaka wa fedha 2024/2025.

“Ninawataka kuwasilisha mkakati utakaoiwezesha Halmashauri kukusanya shilingi milioni 700 zilizobakia hadi kufikia tarehe 31 Juni, 2025 ili kuiwezesha Halmashauri kukusanya mapato kwa asilimia 100 ifikapo tarehe 30 Juni, 2025” amesema Mhe. Mtambi.

Aidha, Mhe. Mtambi pia ametoa siku 90 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kutengeneza barabara ya kuingia katika ofisi za makao makuu ya Halmashauri hiyo ili kuwarahisishia usafiri wananchi wanaofuata huduma katika halmashauri hiyo.

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amewaonya viongozi wa kata na vijiji wanaojihusisha na uvuvi haramu kuchukuliwa hatua za kisheria na kuongeza kuwa nafasi zao sio kichaka cha kuficha uovu huo na Serikali itawachukulia hatua za kisheria.

Mhe. Mtambi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo hali inayoonyesha kuimarika kwa usimamizi na kulitaka Baraza la Madiwani kuendelea kuisimamia vizuri Halmashauri hiyo.  

Kanali Mtambi ameitaka Halmashauri hiyo kuandaa mkakati wa kuweza kutekeleza maagizo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na kujibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wakaguzi.

Mhe. Mtambi ameitaka Halmashauri hiyo kuongeza vyanzo vya ndani vya mapato na kufanya upembuzi yakinifu katika shughuli za uchimbaji madini na uwekezaji uliofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kuifanya halmashauri hiyo kuwa na nguvu ya kiuchumi yitakayowahakikishia ustawi wa wananchi wa Halmashauri hiyo.

Mhe. Mtambi ametoa siku 30 kuanzia leo kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kukamilisha kugawana mali na madeni na kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Bunda kusimamia suala hilo.  

Mhe. Mtambi amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kuandaa vizuri kitabu cha hoja aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kushughulikia hoja ambazo zinasomeka Bunda DC lakini kinachohojiwa kipo Bunda TC na kutoa hadi tarehe 30 Julai, 2025 wataalam wa Halmashauri husika wakutane wazichambue na kuwasilisha taarifa katika ofisi za wakaguzi wa nje.  

Mhe. Mtambi amesema baada ya uchambuzi na makubaliano hayo ya wataalam, hoja husika zitapelekwa katika Halmashauri husika ili ziweze kujibiwa ipasavyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyoge amesema katika Wilaya hiyo kwa sasa kuna tatizo la uvuvi haramu, Wilaya imeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusiana na madhara ya uvuvi haramu katika jamii.

Mhe. Kaminyoge amesema kuna baadhi ya Viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanajihusisha na uvuvi haramu na amewaasa viongozi wa ngazi ya kata na vijiji kuacha tabia ya kujihusisha na uvuvi haramu na Wilaya itafanya operesheni maalum ya kudhibiti uvuvi haramu katika Wilaya hiyo.  

Mhe. Kaminyoge ameahidi kuhamasisha wazazi na walezi kutoa chakula shuleni katika shule zote za Wilaya hiyo baada ya kuanza kwa muhula wa pili wa masomo na kuhakikisha madawati yanapatikana katika shule za msingi na Sekondari na kukarabati shule kongwe zilizopo katika wilaya hiyo.  

Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema Wilaya hiyo inaendelea na maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika tarehe 15 Agosti, 2025 katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na kukabidhi Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mhe.Charles Manumbu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika nchi ya Tanzania.

Mhe. Manumbu amesema kuwa tangu aingie madarakani Halmashauri hiyo imepokea shilingi Bilioni 49 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Mhe. Manumbu ameahidi Baraza la Madiwani litaisimamia Halmashauri kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara.  

Awali akitoa taarifa katika Baraza la Madiwani CPA Denary Gimirey amesema Halmashauri hiyo imepata hati safi ya ukaguzi kwa hesabu za mwaka wa fedha 2023/2024.

CPA Gimirey amesema Halmashauri hiyo pia imepata hati safi katika ukaguzi wa mwaka wa fedha wa 2021/2022, 2022/2023 na 2023/2024.

Bwana Gimirey amesema kuwa taarifa ya ukaguzi unaoishia tarehe 30 Juni, 2024 Halmashauri ilikuwa na jumla ya hoja 99 ambapo 73 hoja za nyuma wakati hoja 26 ni hoja za hesabu za mwaka 2023/2024 baada ya uhakiki hoja 12 zimefungwa na hoja 87 zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.  

Amesema kati ya hoja hizo hoja 58 ni za taarifa kuu, hoja 13 ni za Mfuko wa Pamoja wa Sekta ya Afya na hoja 11 ni za mfuko wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na maagizo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa (LAAC).

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi aipongeza Bunda TC kwa hati safi miaka mitano mfululizo

    June 13, 2025
  • Mtambi aitaka Bunda DC kuwasilisha Mkakati wa kukusanya milioni 700

    June 13, 2025
  • Mtambi aipongeza Halmashauri ya Rorya

    June 12, 2025
  • Mtambi awataka wanawake kugombea nafasi za uongozi

    June 12, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa