Mradi wa USAID Kizazi Hodari unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani (USAID) wenye lengo la kuimarisha afya, ustawi na ulinzi kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na vijana balehe wenye umri wa miaka 0-17 umetambulishwa Mkoa wa Mara tarehe 20 Novemba, 2023.
Akizungumza wakati wa kuutambulisha mradi huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Mradi huo Bibi Vailet Mollel amesema mradi huo unalenga kuwaibua watoto yatima ambao wanakabiliwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI walioko katika maeneo ya migodini, kwenye miala yo uvuvi, pamoja na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Bibi Mollel amesema kwa Mkoa wa Mara mradi huo umelenga kuwahudumia watoto zaidi ya elfu tisa “lengo letu kubwa ni kuwa na kizazi ambacho kina matumaini, uthubutu, na kiko salama dhidi ya changamoto na hatari mbalimbali” aliongeza Bibi Mollel.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Bwana Erick Muhigi amesema mradi huo ni muhimu sana kwa sababu umelenga kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii na ameishukuru Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kuuleta mradi huo katika Mkoa wa Mara.
Bwana Muhigi amezitaja Halmashauri sita zitakazonufaika na Mradi wa Kizazi Hodari kuwa ni Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Halmashauri ya Mji wa Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Kikao cha utambulisho wa mradi huo kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Musoma na kuhudhuriwa na viongozi, wataalamu na wadau mbalimbali.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa