Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa David Ernest Silinde leo tarehe 26 Novemba, 2022 ameanza ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Mara kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu.
Akizungumza katika ziara hiyo ameipongeza Manispaa ya Musoma kwa kujenga majengo ya vyumba vya madarasa yenye ubora unaotakiwa na kwa wakati.
“Mimi ninawapongeza sana kwa kazi kubwa mnayoifanya na hatua mliofikia katika ujenzi mpaka sasa kuna matumaini wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza watakuwa na vyumba vya kusomea” alisema Mheshimiwa Silinde.
Aidha, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondali ya Ifulifu inayojengwa kwa kupitia mradi wa SEQUIP na kuutaka Mkoa wa Mara kutoa taarifa za ukamilishaji wa miradi ya SEQUIP mwishoni mwa Desemba, 2022.
Akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mheshimiwa Silinde amekagua ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Ifulifu na Shule ya Sekondari Suguti ambapo vinajengwa vyumba vitano vya madarasa.
Akiwa katika Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Silinde ametembelea Shule ya Sekondari Buhare (vyumba vitano vya madarasa), Shule ya Sekondari Kiara (vyumba vitano vya madarasa) na Shule ya Sekondari Mwisenge (vyumba 4 vya madarasa).
Akiwa katika ziara hiyo, Mheshimiwa Silinde aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Wakuu wa Idara na Vitengo vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Wakurugenzi wa Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa