Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa David Ernest Silinde leo tarehe 26 Novemba, 2022 anatarajia kuanza ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Mara kukagua ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi Januari, 2023.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara inaonyesha kuwa katika ziara hiyo, Naibu Waziri atatembelea Wilaya za Musoma, Tarime na Bunda.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tarehe 26 Novemba, 2022 ziara ya Mheshimiwa Silinde itaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo atatembelea Shule ya Sekondari ya Ifulifu, Shule ya Sekondari ya Suguti na Shule ya Sekondari ya Makojo wakati akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Silinde atatembelea Shule ya Sekondari ya Buhare, Shule ya Sekondari ya Mwisenge na Shule ya Sekondari ya Kiara.
Tarehe 27 Novemba, 2022 Mheshimiwa Silinde atatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Tarime katika Shule ya Sekondari ya Nyibara, Shule ya Sekondari ya Nyantira na Shule ya Sekondari ya Kemambo. Akiwa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime atatembelea Shule ya Sekondari ya Nyamisangura, Shule ya Sekondari ya Ignana na Shule ya Msingi Turwa kukagua ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mheshimiwa Silinde tarehe 28 Novemba, 2022 atatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bunda katika Shule ya Sekondari Hunyari, Shule ya Sekondari Salama na Shule ya Sekondari Tingirima. Akiwa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda atakagua Shule ya Sekondari ya Bunda, Shule ya Sekondari ya Nyamakokoto.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Silinde ataambatana na viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri husika.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa