• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

Posted on: January 6th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 06 Januari, 2026 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kuagiza mamlaka zote zinazohusika kusimamia usafi wa mazingira kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kudhibiti utupaji hovyo wa taka katika mazingira ya Mkoa wa Mara.  

Mhe. Mtambi amesema kutokana na uwepo wa wanyama wengi katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) na wingi wa mifugo ya wananchi katika Mkoa wa Mara, hivyo kutupa taka hovyo na hususan takataka za plastiki ni hujuma za kiuchumi ambazo zinaweza kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi na Serikali jambo ambalo amesema linaweza kuepukika.

“Baadhi ya taka zinazotupwa ovyo ni mifuko na plastiki na hizi zikiliwa na wanyama hazisagiki tumboni na hivyo kulazimu wanyamapori au mifugo hiyo kufa jambo ambalo linaleta umaskini kwa wananchi mmoja mmoja na Serikali” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) kuhakikisha kuwa wamiliki wote wa mabasi ya abiria yanayofanya shughuli zake katika Mkoa wa Mara kuwa na vyombo vya kuhifadhia taka ndani ya mabasi hayo kwa mujibu wa sheria ili abiria waweze kutupa taka zote ndani ya mabasi.  

Kanali Mtambi amewataka wananchi wa Mkoa wa Mara kuacha mara moja tabia ya kutupa taka ovyo na kuendeleza ustaarabu wa kufanya usafi na kutunza mazingira ili pamoja na mambo mengine kunusuru mifugo na wanyamapori wasife baada ya kula taka za plastiki.  

“Serikali ya Mkoa wa Mara haitamvumilia mtu yoyote anayetupa taka hovyo katika mazingira ya Mkoa wa Mara na kusistiza kuwa usafi wa mazingira utasaidia kufungua fursa katika sekta mbalimbali hususan ufugaji, utalii na kadhalika” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka watumiaji wa barabara kutunza miundombinu ya barabara na kuhakikisha wanazingatia sheria, utaratibu na masharti ya usalama wa barabarani ili Serikali ijikite kuboresha miundombinu ya Mkoa wa Mara na sio kutengeneza miundombinu inayoharibiwa kwa maksudi na watumiaji wa barabara. 

Mhe. Mtambi amesema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) imepata tuzo ya kuwa Hifadhi Bora Duniani kwa miaka mingi mfululizo na ili kunufaika na watalii wanaotembelea hifadhi hiyo katika maeneo ya Mkoa wa Mara, mazingira yake yanatakiwa kuwa safi ili kuwavutia watalii zaidi kuutembelea Mkoa wa Mara.

Kanali Mtambi amewataka watumiaji wa barabara wote kuhakikisha wanatunza miundombinu ya barabara na kuzingatia sheria, taratibu na masharti ya usalama wa barabarani ili kuhakikisha malengo ya Nchi katika kuboresha miundombinu yanafikiwa.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amewakaribisha na kuwapongeza wabunge, Meya na wenyeviti wa Halmashauri kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na wananchi kuwa viongozi waso na kuwahakikishia kuwa kwa sasa ni wajumbe wa kisheri wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutatua kero za wananchi katika maeneo yao.

“Tukifanya kazi kwa umoja na ushirikiano tutafanikiwa zaidi kwani umoja ni nguvu na ushirikiano siku zote huleta mafanikio wakati mapambano na mafarakano yanaishia kwenye uharibifu. Tutekeleze majukumu yetu kwa kushirikiana kati ya watendaji wa serikali na viongozi wa wananchi” alisema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi hao kuwa mabalozi wa kikao hicho na kutoa mrejesho kwa jamii kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao yanayolenga kuondoa changamoto katika jamii na kuwahamasisha wananchi kutunza miundombinu, alama za barabarani, taa na matumizi mabaya ya barabara.

Mhe. Mtambi amesema kwa sasa uchaguzi umepita ni muda wa kujenga uchumi wa mtu mmoja mmoja na Mkoa wa Mara kwa ujumla na kuwahamasisha viongozi pamoja na wananchi wasikubali siasa za kuurudisha nyuma Mkoa na kuwataka wawe na umoja, upendo, mshikamano na kutoa kipaumbele kwa shughuli halali za kiuchumi.  

Kanali Mtambi pia amevishukuru vyombo vya usalama barabarani kwa kufanikiwa kupunguza ajali za barabarani wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2025 na kuwapongeza wananchi kwa kutii sheria za barabarani na kuimarisha amani na utulivu katika maeneo yao.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, wabunge, Meya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara, Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa, maafisa kutoka taasisi za umma, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kiraia.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Mara yaazimia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa