Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Evans Alfred Mtambi ametoa taarifa ya maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakalofanyika Katika Mkoa wa Mara tarehe 4-10 Septemba, 2024.
“Ninawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kutumia haki ya kikatiba kuweza kushiriki katika kuchagua viongozi katika chaguzi zijazo” amesema Bwana Kusaya.
Bwana Kusaya amesema maandalizi yote ya zoezi hili yamekamilika na tayari vifaa vya kuandikishia tayari vimeshasambazwa katika vituo vya 1,597 vitakavyotumika katika Mkoa wa Mara vilivyopo katika majengo ya umma katika vituo maeneo yaliyotumika katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2019/2020.
Bwana Kusaya amesema katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura vituo vya kujiandikishia vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni kwa siku zote saba na kauli mbiu yam waka huu ni “Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora”.
Bwana Kusaya amesema zoezi hili litawahusisha watu wanaojiandikisha kwa mara ya kwanza ambaye anatakiwa kuwa ni raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambaye hakuwa kujiandikisha hapo awali na atakayetimiza miaka 18 ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Aidha, zoezi litawahusisha wananchi wanaoboresha taarifa zaa ambao wamehama eneo la awali alipojiandikishia, taarifa zake za awali zilikosewa na au amepoteza au kadi yake kuharibika na mwananchi aliyepoteza sifa za kuwemo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mfano mtu aliyefariki.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa