Mkoa wa Mara umeanza maandalizi ya kutelekeza miradi ya Elimu na Afya ambayo imeletwa kutokana na fedha za maambikizi ya Uviko 19 na sehemu ya fedha za zilizotokana na tozo.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha wasimamizi wa Mkoa wa miradi ya Elimu na Afya kilichofanyika leo tarehe 18 Oktoba 2021 katika Ukumbi wa Uwekezaji, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi ameeleza kuwa fedha za miradi zilizoletwa wakati huu ni nyingi.
“Haya ni mapinduzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ili kuimarisha huduma za jamii katika maeneo ya Elimu, Afya, Barabara na kadhalika” alisema Mheshimiwa Hapi.
Ameeleza kuwa serikali imeleta shilingi 1,550,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya sita kutokana na fedha za tozo; shilingi 3,190,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya huduma za dharura; na shilingi 1,400,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 618 ya shule za sekondari kupitia Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Mheshimiwa Hapi ameeleza kuwa katika fedha zilizoletwa hamna bajeti ya usimamizi na ufuatiliaji wa mradi hii na hivyo hatarajii watendaji kutumia fedha hizo kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji.
Kikao cha Mkoa cha kujadili utekelezaji wa miradi hiyo kiliazimia kuanzisha mfumo wa kidigitali wa kufuatilia utekelezaji wa miradi yote inayotelezwa ndani ya Mkoa ili kuweza kupata taarifa za miradi hiyo kila siku.
Amewaelekeza Wakurugenzi wa Hamashauri kuhakikisha kuwa madarasa yanayoenda kujengwa kwa kutumia fedha hizo ni mapya na sio kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.
“Tunataka miradi hii ijitegemee na isichanganywe na maboma yaliyojengwa na wananchi au Halmashauri hapo awali” alisema Mheshimiwa Hapi.
Mheshimiwa Hapi amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuunda kamati za ujenzi ndani ya wiki hii na kuanza kutafuta sehemu ya kupata vifaa vya ujenzi wakati wakisubiri maelekezo kuhusu matumizi ya fedha hizo kutoka serikalini.
Amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakrugenzi wa Halmashauri kuwatangazia vijana fursa zinazotokana na miradi hii katika maeneo yao ili waweze kuchangamkia fursa hizo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa