Mkoa wa Mara umeshika nafasi ya kumi Kitaifa kwa wingi wa idadi ya watu katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 iliyotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 31 Oktoba, 2022.
Katika matokeo hayo Mkoa wa Mara umekuwa ni Mkoa wa kumi Kitaifa ukiwa na jumla ya watu 2,372,015 ambapo kati ya watu wote waliopo wanaume ni 1,139,511 na wanawake ni 1,232,504.
Mkoa unaoongoza kwa idadi ya watu ni Dar es Salaam (5,383,728), ukifuatiwa na Mkoa wa Mwanza (3,699,872), Mkoa wa Tabora (3,391,679), Mkoa wa Morogoro (3,197,104), Mkoa wa Dodoma (3,085,625) na Mkoa wa Kagera (2,989,299).
Mikoa mingine yenye idadi kubwa ya watu ni Mkoa wa Geita (2,977,608), Mkoa wa Tanga (2,615,597), Mkoa wa Kigoma (2,470,967) na kufuatiwa na Mkoa wa Mara ambao kwa mujibu wa matokeo hayo umewazidi kwa idadi ya watu mikoa mingine yote iliyobakia.
Aidha kwa Tanzania Bara Mkoa wenye idadi ndogo ya watu ni Njombe wenye jumla ya watu 889,946 ukifuatiwa na Mkoa wa Katavi (1,152,958), Mkoa wa Iringa (1,192,728) na Mkoa wa Lindi wenye watu 1,194,028.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo hayo, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa kuwa Tanzania ina jumla ya watu 61,741,120 ambapo kati yao wanawake ni 31,687,990 ambao ni asilimia 51 huku wanaume wakiwa 30,053,130 ambao ni sawa na asilimia 41 ya watu wote.
Mheshimiwa Samia ameeleza kuwa kati ya watanzania wote waliohesabiwa, Tanzania Bara wapo 59,851,347 huku Tanzania Zanzibar ikiwa na jumla ya watu 1,889,773.
Aidha, Mheshimiwa Rais amesema kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru Tanzania imefanikiwa kufapata taarifa za majengo na anuani ya makazi, taarifa hizi zina umuhimu mkubwa wa kufuatilia na kutathmini sera za mipango miji hapa nchini.
Aidha, taarifa hiyo ineonyesha kuwa vituo vya kutolea huduma za afya 10,067 majengo yote 14,348,372 na kati ya hayo Tanzania Bara yapo 13,907,951 na Tanzania Zanzibar yapo 440,421 wakati shule zikiwa 25,626.
Msheshimiwa Samia ametoa pongezi kwa wananchi wote kwa kutoa ushirikiano wao kufanikisha zoezi la sensa na kamati za ngazi zote zilizofanikisha zoezi la sensa hapa nchini.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa