Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee leo ameeleza kuwa Mkoa wa Mara umejipanga kuhakikisha hakutakuwa na matukio ya uvunjifu wa amani na kuzua taharuki wakati wote wa sikukuu za mwaka mpya.
Mheshimiwa Mzee ametoa tamko hilo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya sikukuu yam waka mpya, 2023.
“Sisi Mara tumejipanga kuhakikisha Mkoa unakuwa na amani wakati wote wa sikukuu na vyombo vyote vya ulinzi na usalama vimejipanga kukabiliana na uhalifu wowote unaoweza kutokea wakati huu” amesema Mheshimiwa Mzee.
Mheshimiwa Mzee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa Mkoa hautaruhusu matukio yoyote ya vurugu za kuchoma matairi, kurusha fataki na mengine yanayoweza kuleta taharuki kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa pia amewatakia heri ya sikukuu Watanzania wote na kuwataka waendelee kufanya shughuli zao za kila siku wakiwa na amani na utulivu.
Mheshimiwa Mzee amewakaribisha watanzania wote pamoja na wageni kuutembelea Mkoa wa Mara wakati huu wa sikukuu na hususan Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na fukwe za Ziwa Victoria ili kuweza kufurahia na ndugu na marafiki zao wakati huu wa sikukuu.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa