Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhehsimiwa Adam Kighoma Ali Malima ameipongeza halmashauri ya Mji wa Tarime kwa kufanya vizuri kwa mujibu wa ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Mheshimiwa Malima ametoa pongezi hizo leo tarehe 9 Juni 2020 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za CAG kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kilichofanyika katika
“Mimi ninawapongeza sana kwa mujibu wa taarifa hii mnafanya vizuri sana lakini pia taarifa inaonyesha mnaweza kufanya vizuri zaidi kwa sababu baadhi ya hoja zilizotolewa ni za kawaida sana hazikutakiwa kuwepo hapa” alisema Malima.
Aidha aliitaka halmashauri hiyo kuongeza matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo ya halmashauri hiyo ilikuweza kuwanufaisha wananchi.
“Mnatakiwa kuweka asilimia 40 na maana yake itumike pia asilimia 40 na sio asilimia 25 kama mlivyofanya nyinyi” alisema Malima.
Mheshimiwa Malima amewapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kuisimamia vizuri halmashauri hiyo pamoja na kuwa ni wachache sana. Aidha ameeleza kuwa anawaombea madiwani hao kwa Mungu ili waweze kurudi katika nafasi zao baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kwa mwaka 2018/2019 Halmashauri ya Mji wa Tarime ilipata hati safi na ilikuwa na hoja 29 za zamani na hoja 19 mpya.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa