Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, RaphaelJoseph Nyanda, amewakumbusha Maafisa Habari na Maafisa wa Teknolojia ya Habarina Mawasiliano (TEHAMA) nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi,maarifa na ubunifu, kwakuwa wao ni mawakala wa mabadiliko.
Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilichoandaliwa naOfisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwakushirikiana na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), NduguNyanda amewatahadharisha maafisa hao kuwa endapo watazembea kutekeleza wajibuwao wa msingi kwa weledi, watu wengine watapotosha umma.
“Kilammoja miongoni mwenu anayo dhamana ya kutangaza mambo mazuri yanayofanywa naSerikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu, watu wasio wemawatapotosha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya Serikali”amesisitiza Nyanda.
Akizungumzawakati wa kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Bi Rebbeca Kwandu, amewasisitizia maafisa hao kubadilika katika utendaji waomara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.
“Mwanzonitulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na mwongozo ambao ni dira yauendeshaji. Hata hivyo mara baada ya OR-TAMISEMI kuandaa mwongozo huu kwakushirikiana na wadau wetu PS3, ni imani yangu tutabadilika,” alisema Bi.Kwandu, na kuongeza kwamba uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.
Akizungumzakwa niaba ya Mradi wa PS3, Mkuu wa Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Wananchi,Dkt. Peter Kilima, amekiri kwamba Maafisa Habari na Maafisa TEHAMA ndio roho yataasisi, hivyo ushirikishwaji hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursakwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.
Awaliakitoa Salaam za Idara ya Habari (Maelezo), Mkurugenzi Msaidizi wa Habari naPicha, Rodney Thadeus, aliesema kwamba ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywana Serikali, ni lazima Maafisa Habari wawe na zana za utendaji kazi, na zanazenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa ni tovuti.
“WafadhaliPS3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Framework (GWF). Tumieni hizi tovuti kama tools (zana) za kuujuzaumma.
Mafunzohaya ya siku nne ni ya awamu ya kwanza kwa Maafisa Habari na Maafisa TEHAMAkutoka mikoa ya Mara na Arusha, na mafunzo kama haya yatafanywa pia kwa maafisakutoka mikoa mingine yote iliyobaki ya Tanzania bara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa