Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo inatarajia kuwasili Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuanza ziara katika Mkoa wa Mara ambapo itatembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya za Tarime, Serengeti, Musoma na Butiama.
Ratiba ya ziara hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inaonyesha kuwa kesho kamati hiyo itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala na Shule ya Sekondari ya Nyasarisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, tarehe 22 Machi, 2024 Kamati ya LAAC itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala na soko la kimkakati katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Tarehe 23 Machi, 2024, Kamati hiyo itaelekea Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambapo itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti na baadaye kuondoka kuelekea Manispaa ya Musoma.
Tarehe 24 Machi, 2024, Kamati itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Rwamlimi na mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kigera katika Manispaa ya Musoma.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Kamati itahitimisha ziara yake katika Mkoa wa Mara tarehe 25 Machi, 2024 kwa kufanya ziara katika Wilaya ya Butiama ambapo itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kamugegi na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Butiama.
Maandalizi kwa ajili ya ziara ya Kamati ya LAAC katika Mkoa wa Mara yamekamilika.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa