• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

Posted on: May 30th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo ameshiriki maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kuwataka wauguzi kuishi viapo vyao wanapotoa huduma kwa wananchi.

Ndugu Kusaya amesema wauguzi wameapa mbele ya umma kutoa huduma bora na kuongeza kuwa kauli mbiu ya siku ya waguuzi mwaka huu ni “Uuguzi ni nguvu ya kuleta Mabadiliko Duniani” na kuwataaka kuiishi kauli hiyo kwa vitendo ili kuokoa maisha ya wananchi.

“Viapo vyenu ambavyo mnakuwa mnavirudia mara kwa mara ni vizuri sana na kama mkiviishi kwa vitendo vitaokoa maisha ya wananchi wengi katika maeneo yenu” amesema Bwana Kusaya.

Ndugu Kusaya amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa afya wakiwemo wauguzi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuyafanyia kazi mambo mbalimbali wanayoelekeza katika jamii ikiwemo kuzingatia lishe, usafi wa mazingira na kufanya mazoezi.

Akizungumzia kuhusu upungufu wa watumishi Ndugu Kusaya amesema upungufu wa watumishi upo katika sekta mbalimbali sio sekta ya afya pekee na kuongeza kuwa kwa sasa Mkoa wa Mara unahitaji watumishi 15,441 wa kada mbalimbali.

“Serikali imekuwa ikiajiri watumishi mara kwa mara na kwa mwaka huu pekee Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imepokea watumishi 170 na kati yao watumishi 48 wakiwa wa sekta ya afya” amesema Bwana Kusaya.

Aidha, Bwana Kusaya amesema Halmashauri imepokea kibali cha ajira kwa watumishi 40 na baadhi yao watakuwa ni wa sekta ya afya wakiwemo wauguzi.

Bwana Kusaya ametumia fursa hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kwa kutenga shilingi milioni 50 kwa mwaka kwa ajili ya kununua vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya.

Bwana Kusaya ametumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wananchi na watumishi kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwataka watumishi wanaotaka kugombea katika uchaguzi huo kufuata taratibu za kiutumishi kuaga ili waweze kuruhusiwa kuondoka.  

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Bwana Msongera Palera amesema Halmashauri inaupungufu wa watumishi lakini Serikali imekuwa ikileta watumishi kila mwaka kutatua changamoto hiyo.

Bwana Palera amelishukuru Baraza la Madiwani kwa ushirikiano na maamuzi mazuri wanayotoa na kuwapongeza wauguzi kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwahakikishia watumishi wenye madai ya malimbikizo ya mshahara madai yao yapo katika hatua nzuri muda wowote wanaweza kulipwa.

Bwana Palera amesema kuhusu malipo ya posho, unifomu na stahiki nyingine ameviachia vituo ili vilipe kulingana na makusanyo katika vituo na kuwataka watumishi kuboresha huduma zao ili kuongeza makusanyo.  

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mhe. Mussa Munubi amemuomba Katibu Tawala wa Mkoa kuisaidia Halmashauri katika kutatua tatizo la watumishi wa sekta ya afya katika Halmashauri hiyo.

“Mahitaji ni watumishi 223 na kwa sasa waliopo ni watumishi 104 tu na hivyo kuna upungufu wa watumishi 119 na upungufu mkubwa ukiwepo hapa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma” amesema Mhe. Munubi.

Mhe. Munubi amewapongeza watumishi kwa kazi nzuri wanayoifanya pamoja na uchache wao na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuokoa maisha ya wananchi wa Musoma wanaotegemea huduma za afya kutoka kwa wataalamu hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANA) Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Bibi Nice Mremi amesema wauguzi ndio wataalamu wanaompokea mgonjwa na wataalamu wa mwisho kuagana na mgonjwa na kuiomba Serikali kuwaboreshea mazingira yao ya kufanyia kazi.

Bibi Mremi ameomba Serikali kuongeza idadi ya watumishi na hususan Hospitali ya Halmashauri, vitendea kazi, fedha za sare, likizo na posho zitolewe kwa wakati, kuboresha baadhi ya vituo vya kutolea huduma.

Kwa upande wake, Bwana Ndulu Mahera, Mratibu wa Maabara Halmashauri ya Wilaya ya Musoma amesema katika kuadhimisha wiki ya wauguzi, Halmashauri iliweka mahema na kufanya upimaji wa baadhi ya magonjwa na kutoa chanjo na ushauri nasaha kwa wananchi katika viwanja hivyo.

Bwana Mahera amesema wamefanikiwa kuhamasisha wananchi 46 kuchangia damu, wamepima UKIMWI watu 45, wametoa chanjo mbalimbali kwa watoto na kutoa ushauri kuhusiana na uzazi wa mpango kwa wananchi.

Katika maadhimisho hayo, Katibu Tawala amezindua kampeni ya lishe katika Halmashauri hiyo, amegawa zawadi kwa wagonjwa zilizotolewa na waauguzi na ameendesha harambee fupi ya kutunisha mfuko wa Chama cha Wauguzi.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na baadhi ya Watumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na wananchi wa maeneo hayo.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • Waongozeni wanafunzi kufikia ndoto zao- Kusaya

    May 29, 2025
  • Kamati za Maafa Mkoa wa Mara zajengewa Uwezo

    May 26, 2025
  • Kikwete achangisha milioni 200 za ujenzi wa kanisa Mara

    May 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa