• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kusaya ateta na viongozi wa Bodi ya Mkonge

Posted on: August 14th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo amempokea na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania Ndugu Sady H. Kambona aliyetembelea ofisini kwake  ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha kilimo cha zao la mkonge katika Mkoa wa Mara.

Akizungumza na ugeni huo, Ndugu Musabila amesema wakulima wa Mkoa wa Mara wapo tayari kuwekeza katika kilimo cha mkonge kama watapata uhakika wa soko la zao hilo bila ya kulazimika kuvusha kwa magendo kwenda katika nchi jirani kutafuta masoko.

“Soko la mkonge likiwa ni la uhakika hapa nchini litahamasisha wakulima wengi zaidi kuwekeza katika kilimo cha mkonge na kuwasaidia kuuza kwa bei nzuri kuliko hivi sasa ambapo Mkoa hauna soko la uhakika la mkonge” amesema Bwana Kusaya.

Ndugu Kusaya amesema kutokana na hali ya hewa ya Mkoa wa Mara mkonge unaweza kustawi vizuri  hususan katika Wilaya ya Bunda ambayo ina hali ya ukame muda mwingi jambo ambalo linaweza kuufanya mkonge kuwa zao kuu la biashara kwa wakulima.

Bwana Kusaya ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya zao la mkonge kwa mikoa mbalimbali inayoweza kulima zao hilo ili kujionea hali halisi iliyopo katika maeneo hayo na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.

Kwa upande wake, Bwana Kambona amesema kuwa kwa sasa kwa sababu wakulima wa Mkoa wa Mara wanauza mkonge kiholela Halmashauri za Mkoa wa Mara zitakuwa hazinufaiki na kilimo cha mkonge kwa kuwa hazikusanyi mapato yanayotokana na uuzaji wa zao la mkonge.

Bwana Kambona ameshauri Halmashauri kutunga sheria ndogo ili kuweza kunufaika katika kilimo cha zao la mkonge na kuwahamasisha wakulima kuwekeza katika zao hilo ambalo amesema mbali na kutoa nyuzi za mkonge mabaki yake yanaweza kutengenezwa na kuwa chakula cha mifugo na hivyo kuongeza thamani zaidi ya zao hilo.

Ndugu Kambona amesema kwa sasa Serikali imewekeza katika kuanzisha vituo vya uzalishaji na kuunda vyama vya ushirika vya wakulima wa mkonge na kuwawezesha wakulima hata wa kiasi kidogo kufaidika na mkonge wao.  

Ndugu Kambona ameutaka Mkoa wa Mara kwa kuanzia kuwahamasisha wakulima kupanda mikonge katika mipaka ya mashamba yao ili kufaidika na mauzo ya zao hilo huku likilinda mipaka ya mashamba yao.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mhandisi Mwita Okayo amesema Mkoa wa Mara unao wakulima wa zao la mkonge hata hivyo kutokana na kukosekana kwa soko la uhakika wakulima hao wanauza mkonge wao kwa njia za magendo katika nchi jirani.

Mhandisi Okayo amesema wakulima wa Mkoa wa Mara baada ya kuhamasishwa mwaka 2011 kulima zao la mkonge waliitikia wito hata hivyo hamna wanunuzi wa zao hilo waliokuwa wananunua mkonge katika Mkoa wa Mara na hivyo kuwakatisha tamaa wakulima zaidi kulima zao hilo.

Mhandisi Okayo amezitaja Wilaya ambazo zinalima mkonge kuwa ni pamoja na Rorya, Bunda, Butiama, Tarime na Serengeti ambazo zina wakulima wadogo wadogo wengi na kumtaka kiongozi huyo wa Bodi ya Mkonge kukutana na wakulima ili kuwatia moyo kuhusu upatikanaji wa soko la uhakika na jitihada za bodi hiyo kuinua zao hilo katika Mkoa wa Mara.

Mhandisi Okayo ameiomba bodi hiyo kujenga kituo cha kuzalishia mkonge katika Wilaya ya Butiama ili wakulima wa Mkoa wa Mara waweze kupata urahisi wa kuuza mkonge wao. 

Katika kikao hicho, Bwana Kambona aliambatana na Afisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Mkonge na mmoja wa wanunuzi wa zao la mkonge ambaye amefanya ziara ili kujionea hali halisi ya soko la mkonge katika Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Mara yapokea mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 15, 2025
  • Kusaya ateta na viongozi wa Bodi ya Mkonge

    August 14, 2025
  • Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya bilioni 26.6 Mara

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa