• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

Posted on: August 18th, 2025

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi leo tarehe 18 Agosti, 2025 ameongoza tukio la Mwenge wa Uhuru kuwasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarege Ntyerere, eneo la Mwitongo, Butiama.

Ndugu Ussi amewasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61 tangu mbio za mwenge wa Uhuru zilivyoanzishwa mwaka 1964 huku akiwa ameambatana na wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, wazee wa kimila na familia ya Mwalimu Nyerere.

Nyumbani kwa Baba wa Taifa viongozi wa Mwenge wa Uhuru wamepata taarifa za kihistoria kuhusu Mwenge wa Mwitongo, Baba wa Taifa na familia yake pamoja na kuzuru kaburi la Baba wa Taifa na kuweka mashada na kutembelea Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama.

Nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwenge umepokelewa na wanafamilia wa Mwalimu Nyerere wakiongozwa na Chifu Japheti Wanzagi kiongozi wa familia ya Mwalimu Nyerere na kiongozi wa kabila la Wazanaki.

Wakati huo huo, Mwenge wa Uhuru umepitia miradi nane ya maendeleo katika Wilaya ya Butiama yenye thamani ya shilingi 3,767,195,293.00 na kati ya gharama hizo fedha za wananchi ni shilingi 1,288,582,500.00; mchango wa Halmashauri ni shilingi 45,000,000.00 na fedha za Serikali Kuu ni 2,433, 612,793.00.

Baada ya kupokelewa katika uwanja wa Shule ya Msingi Nyabange, Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi Kituo cha Afya Wegero; umefungua Shule ya Sekondari ya Sirorisimba na kukagua upandaji wa miti katika eneo hilo; umezindua kituo cha mafuta Isaka; na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa mtandao wa maji wa Kijiji cha Nyambili.

Aidha, Mwenge wa Uhuru umezindua daraja la Buturu- Mwanzaburiga na kutembelea mradi wa vijana waendesha bodaboda eneo la Nyasirori na kuweka jiwe la msingi mradi wa machinjio ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.

Mwenge wa Uhuru umehitimisha mbio zake katika Uwanja wa Mwenge Butiama ambapo mkesha wa Mwenge wa Uhuru unaendelea. Ukiwa katika eneo la mkesha, Mwenge wa Uhuru utakagua kongamano la vijana; shughuli za lishe; kukagua shughuli za kuzuia na kupambana na rushwa; kupokea taarifa za maandalizi ya uchaguzi; kukagua utoaji wa elimu na shughuli za kuzuia dawa za kulevya; kukagua mabanda ya wajasiriamali na kupokea risala ya utii.  

Kesho tarehe 19 Agosti, 2025 Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuendelea na mbio zake katika Wilaya ya Rorya ambapo makabidhiano yatafanyika katika eneo la Kinesi.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • Mwenge wakagua miradi ya bilioni 6 Musoma

    August 18, 2025
  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Mara yapokea mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa