Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Adam Kighoma Malima ameonya dhidi ya matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa miradi ya barabara zinazojengwa Mkoani Mara. Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa kikao cha RCC ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. Katika kuonesha msisitioz na kumaanisha anachosema Mkuu wa Mkoa alisema '' vitendo vya rushwa ni moja ya sababu kubwa sana inayosababisha fedha kutumiwa hovyo na miradi kutokamilika kwa wakati''. Hali hii inazorotesha maendeleo. Mkuu wa Mkoa alizidi kusisitiza ni bora fedha hizo zipelekwe kwenye miradi mingine ya maendeleo kuliko kutumiwa kujenga barabara ambazo hazina ubora nafedha nyingi kupotea mikononi mwa watu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka watendaji wote wa Mkoa kuweka mipango na kuhakikisha wanaitekeleza kama ilivyopangwa ili kuweza kuwahudumia wananchi.Ili kutimiza azma ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ya kujenga uchumi wa kati kufikia 2025 ameonya vitendo vya rushwa, uvivu, ubadhilifu wa mali za Umma . Amesisitiza kila mtumishi kuwajibika ipasavyo ili kuweza kutimiza malengo ya Serikali ya kuwakomboa wananchi wanyonge.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa