• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kamati ya Usalama Mkoa yatembelea eneo la maafa Manispaa ya Musoma

Posted on: March 25th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi akiwa ameongozana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara leo tarehe 25 Machi, 2025 ametembelea eneo lililokumbwa na maafa katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na kujionea uharibifu  uliotokea kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali tarehe 23 Machi, 2025 usiku.

“ Nimekuja hapa nikiwa  nimeongozana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Katibu wa chama cha mapinduzi, viongozi na wataalamu mbalimbali kutoka mkoani, Manispaa ya Musoma kuwapa pole, kuangalia hali halisi ilivyo na kutoa msaada wa haraka unaohitajika” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewapongeza wananchi wa Manispaa ya Musoma kwa kuwasaidia walioathirika katika maafa hayo, kuwahi kutoa taarifa kwa vyomba vya Usalama na viongozi mbalimbali na kuzipongeza taasisi zote zilizosaidia katika kufanya uokoaji wa haraka katika maeneo mbalimbali.

Akiwa katika eneo hilo, Mhe. Mtambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kukarabati mara moja nyumba ya Bibi Eveline Masuba mkazi wa mtaa wa Makongoro uliopo katika kata ya kitaji ambaye paa la nyumba yake pia limeezuliwa na upepo huo.

Aidha, ameiagiza Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Musoma kuongeza ulinzi katika maeneo yote yaliyoathirika na maafa hayo ili wananchi na mali zao waweze kuwa salama.

Mhe. Mtambi amewatahadharisha wezi na watu wote waliojipanga kuiba katika kipindi hiki cha maafa kwa kuwajulisha kuwa Kamati ya Usalama Mkoa na Wilaya zimejipanga kuimarisha ulinzi na yeyote anayepanga kuiba au kuharibu mali za wananchi na taasisi za umma atakamatwa.

Mhe. Mtambi amewahakikishia wananchi kuwa timu mbalimbali za wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Manispaa ya Musoma zitapita katika maeneo yao ili kufanya tathmini na kutoa msaada wa dharura unaohitajika katika maeneo hayo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa timu hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Mrakibu Agustine Magere amesema maeneo yaliyoathirika ni kata 10 za Manispaa ya Musoma ambazo ni;  Kitaji, Iringo, Mwigobelo, Kamunyonge, Mukendo, Mwisenge, Kwangwa, Bweri, Rwamlimi na Nyakato.

Kamanda Magere amesema kutokana na athari ya tukio hilo, kikosi kiliamua kuifunga barabara ya Lumumba Manispaa ya Musoma baada ya nyaya na nguzo za umeme kuangukia katika barabara hiyo na kuzuia maeneo ya starehe yaliyoathirika katika tukio hilo kuendelea kutumika hadi hapo yatakapopewa idhini na Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma baada ya kujiridhisha kuhusu usalama wake.

Bwana Magere amesema jumla ya watu wanne walijeruhiwa katika maafa hayo kutoka katika Kata ya Kitaji na watatu wakiwa ni wavulana wenye miaka 3-12 na mmoja mwanamke (43) na wote walipatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya.

Kamanda Magere amesema wananchi ambao makazi yao yameathirika wameshauriwa kuhama katika maeneo hayo na kutafuta makazi ya muda wakati wakiendelea kuyarejeshea majengo yao katika hali yake ya kawaida na kuwataka wananchi kupiga namba ya bure ya kikosi hicho 114 ili kupata msaada wa haraka kunapotokea ajali au majanga.

Vilevile, Kamanda Magere amesema tukio hilo limeathiri miundombinu mbalimbali ya Manispaa ya Musoma ikiwemo barabara, miundombinu ya maji na umeme na imeharibu majengo ya taasisi mbalimbali ikiwemo ofisi za TANESCO, ofisi ya TTCL Mkoa wa Mara, majengo ya biashara na kuhudumia abiria katika Uwanja wa Ndege Musoma.

Majengo mengine ni majengo ya shule tano za msingi ikiwemo bweni moja la wanafunzi wenye mahitaji maalum lililokuwa linajengwa na mfadhili Shirika la Support Build for Student with Disability, Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kitaji, Kanisa Katoliki, Msikiti katika eneo la Iringo na Kituo cha Polisi Kitaji. 

Kamanda Magere amesema katika tukio hilo pia baadhi ya maeneo ya biashara kama vile maduka, kumbi za starehe, kituo cha mafuta (TANOIL) kilichopo Barabara ya Uhuru nacho kiliathiriwa na tukio hilo.

Aidha, jumla ya kaya 319 kutoka Kata 10 za Manispaa ya Musoma zimeathiriwa na tukio hilo lililotokea tarehe 23 Machi, 2025 na jitihada mbalimbali za kurejesha hali ilivyokuwa na usalama wa wananchi katika eneo hilo zinaendelea.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC azitaka Wilaya kuongeza nguvu maandalizi ya Mwenge 2025

    May 09, 2025
  • Mtambi akabidhi tuzo na kinyago washindi wa Mwenge 2024

    May 09, 2025
  • Mtambi alitaka jukwaa la ushirika kuongeza ubunifu

    May 08, 2025
  • Jumuiya ya Waislamu Musoma yachangia madawati

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa