• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DC Chikoka afungua semina ya michongo kwa maafisa usafirishaji Musoma

Posted on: December 3rd, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikako leo tarehe 03 Desemba, 2025 amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara katika uzinduzi wa Semina michongo (fursa) iliyotolewa kwa maafisa usafirishaji wa Manispaa ya Musoma uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhe. Chikoka amesema lengo la semina hiyo ni kuwapatia fursa za kiuchumi zitakazoweza kuwaongezea kipato maafisa usafirishaji hao na kuwataka kuachana na vitendo vinavyoweza kuhatarisha Amani.

“Ndugu zangu michongo hii mkiizingatia mnaweza kufanikiwa kiuchumi ninyi na familia zenu na kuimarisha uchumi wa Taifa letu” amesema Mhe. Chikoka na kuwataka maafisa usafirishaji hao kuchangamkia fursa zilizopo ili kuboresha maisha yao.

Mhe. Chikoka amezitaja fursa zilizopo ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, mafunzo ya udereva yaliyopunguzwa bei yatakayotolewa na Chuo cha VETA Mara na bima mbalimbali ambazo amesema Serikali imezitoa kwao na hivyo wakitaka kubadili maisha yao wazichangamkie fursa hizo  zitakazoanza kutolewa kuanzia tarehe 5 Desemba, 2025.

Mhe. Chikoka amewataka maafisa usafirishaji hao ambao wanajumuisha madereva wa pikipiki na bajaji  kuwa mabalozi wa amani na kuacha kujihusisha na vitendo ambavyo vinavyochochea uvunjifu wa amani katika Mkoa wa Mara.

“Maandamano sio dili, dili ni michongo ya maendeleo itakayowawezesha kujikwamua kiuchumia” amesema Mhe. Chikoka na kuongeza kuwa semina hiyo itawasaidia kuzifahamu fursa zilizopo na kuzichangamkia.   

Mhe. Chikoka amesema kwa sasa Serikali inaimarisha miundombinu ya usafirishaji katika Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi ya Bweri, barabara, uwanja wa ndege wa Musoma na Serengeti na kadhalika ili kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Musoma amesema benki hiyo inatoa mikopo yenye riba nafuu ikiwemo mikopo ya pikipiki ambapo mkopaji anachangia asilimia 20 ya thamani ya pikipiki hiyo pamoja na mikopo ya fedha taslimu zinazotolewa kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

Meneja huyo amewashauri Maafisa Usafirishaji hao kufungua akaunti ya NMB Pesa ili kuweza kuwarahisishia upatikanaji wa mikopo inayotolewa na benki hiyo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa LATRA amewataka maafisa usafirishaji hao kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani.

 Taasisi zilizoshiriki katika semina hiyo ni pamoja na Shirika la Bima la Taifa (NIC), Benki ya NBC, Benki ya NMB, Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) na taasisi nyingine.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awataka wananchi kuchangamkia fursa ya kupima saratani bure

    December 04, 2025
  • DC Chikoka afungua semina ya michongo kwa maafisa usafirishaji Musoma

    December 03, 2025
  • RC Mtambi awataka viongozi wa dini kuwahamasisha wananchi kuilinda Tanzania

    December 01, 2025
  • Kusaya aridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mara

    November 27, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa