Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara imeandaa Bonanza la Michezo kwa watumishi wa taasisi za umma na taasisi binafsi kesho tarehe 22 Februari 2020 katika uwanja wa Karume uliopo Musoma Mjini.
Akizungumzia maandalizi Bwana Evance Sangawe ambaye ndiye mratibu wa bonanza hilo amesema bonanza litahusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, netiboli, mpira wa wavu, riadha mita 100, 200, 400 na 800, mbio za magunia na kuvuta kamba.
“Bonanza litaanza saa 12:15 asubuhi kwa kukimbia kuanzia uwanja wa Mukendo na kuzunguka katikati ya mitaa ya Manispaa ya Musoma na kuhitimishwa katika uwanja wa Karume saa 1.05 asubuhi” alisema Bwana Sangawe. Ameeleza pia kuwa mashindano ya michezo yatakayohusisha timu mbalimbali yataanza saa 1.30 Asubuhi.
Bwana Sangawe amesema pia kuwa timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara inaendelea kujifua na mashindano hayo na inategemea kunyakua vikombe vingi zaidi ukilinganisha na bonanza lililopita. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Tawala wa Mkao wa Mara
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa